Pata taarifa kuu
HAKI ZA WANYAMA

Tembo aliyedhulumiwa katikati mwa mzozo wa kidiplomasia kati ya Thailand na Sri Lanka

Tembo wa Thailand ambaye alikuwa amepewa kama zawadi nchini Sri Lanka alirejeshwa Jumapili Julai 2 katika ardhi yake ya asili katikati mwa shutma za kufanyiwa dhulma na kutendewa vibaya.

Daktari wa mifugo anajishughulisha na matibabu ya tembo Sak Surin, katika Bustani ya Kitaifa ya Wanyama huko Colombo, Sri Lanka, Ijumaa, Juni 30, 2023.
Daktari wa mifugo anajishughulisha na matibabu ya tembo Sak Surin, katika Bustani ya Kitaifa ya Wanyama huko Colombo, Sri Lanka, Ijumaa, Juni 30, 2023. AP - Eranga Jayawardena
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Bangkok, Carole Isoux

Tembo huyo aliyepewa jina la Sak Surin, 29, heshima ya mkoa wa Thai wa Surin, maarufu kwa tembo wake, ilitolewa kwa Sri Lanka kama zawadi mnamo mwaka 2001 na kuitwa Muthu Raja, katika lugha ya Kitamil, "mfalme wa rangi ya lulu".

Lakini mwaka jana, wanaharakati walishutumu hali ya kusikitisha ya mnyama anayetumiwa katika vibarua katika tasnia ya mbao na hekalu la Wabuddha. Mwili wake ulikuwa umetapakaa majipu na kuonyesha alama za vipigo. Thailand basi mara moja ilidai kurejeshwa kwa mnyama huyo, licha ya maandamano ya wanaharakati wa Sri Lanka ambao walipenda wamhudumie wenyewe Muthu Raja (tembo huyo) huko Sri Lanka, ambapo sheria kali hudhibiti unyanyasaji wa tembo.

Mnyama aliyetakaswa

Kesi hiyo ilizua taharuki kubwa, kwani Waziri Mkuu wa Sri Lanka aliomba msamaha kwa Mfalme wa Thailand, ambapo tembo anachukuliwa kuwa mnyama aliyetakaswa, ishara ya kifalme na utambulisho wa kitaifa.

Baada ya safari ya saa tano kwa ndege akiwa na daktari wa mifugo na wakufunzi kadhaa kutoka Thailand na Sri Lanka, tembo huyo aliwasili Chiang Mai akiwa na afya njema ambapo atapelekwa katika hifadhi yake ya asili. Waziri wa Mazingira alikuwepo kuwapokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.