Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Thailand: Pita Limjaroenrat kuwani kwenye nafasi ya waziri mkuu ni kinyume na sheria

Sntofahamu yatanda nchini Thailand. Kura ya kumchagua Waziri Mkuu mpya ilikuwa ifanyike Jumatano hii, Julai 19. Lakini katika hali ya kushangaza, Mahakama ya Katiba imesitisha mbio za mbunge huyu katika kinyang'anyiro cha kuwani nafasi hii, ambaye alikuwa mgombea pekee katika nafasi ya waziri mkuu.

Thailand, Julai 19, 2023: Baada ya kugombea kwake kwenye wadhifa wa Waziri Mkuu kutangazwa kuwa ni kinyume cha sheria, Pita liondoka bungeni akipigiwa makofi, huku akiinua mkono juu na kusema "nitarudi".
Thailand, Julai 19, 2023: Baada ya kugombea kwake kwenye wadhifa wa Waziri Mkuu kutangazwa kuwa ni kinyume cha sheria, Pita liondoka bungeni akipigiwa makofi, huku akiinua mkono juu na kusema "nitarudi". AP - Sakchai Lalit
Matangazo ya kibiashara

Pita, ni kiongozi kijana na mwenye mvuto wa chama cha Move Forward, mshindi mkubwa wa uchaguzi wa Mei mwaka huu. Kufuatia uamuzi huu, wengi wa maseneta na wabunge walimzuia kwa kutangaza kuwania kwake ni kinyume cha sheria.

"Pita haiwezi kuteuliwa mara mbili katika kikao hiki cha Bunge," chini ya Ibara ya 41 ya Kanuni za Uendeshaji za Bunge, rais wa Bunge la Seneti amesema, kufuatia kura ya mabunge yote mawili.

Kwa hiyo Pita hawezi kuwania kwa mara ya pili. Muda mfupi kabla ya kura hii ambayo haikutarajiwa, Pita aliondoka bungeni akipigiwa makofi, huku akiinua mkono juu na kusema "nitarudi". Kuondoka kwake, hata hivyo, kunaonekana kama mwisho wa  ndo za vijana, ambao walipiga kura nyingi kwa chama chake cha Move Forward.

Mbele ya kusanyiko huko Bangkok, mamia ya waandamanaji wamekusanyika kutaka sauti zao zisikike na viongozi waliochaguliwa, anaripoti mwandishi wetu huko Bangkok, Carol Isoux. Wana hasira na wasiwasi kama vile Tole Manuchai ni mwalimu wa shule huko Bangkok: kwake yeye, taratibu hizi zote ni shani za upinzani unaounga mkono jeshi. "Kwangu mimi, ni wazi, wanajaribu kupoteza wakati ili kuchelewesha iwezekanavyo zoezi hili wakati ambapo serikali nyingine itaingia madarakani, kwa kudharau matokeo ya kura ya raia wa Thailand, ambayo yalitoa nafasi ya wazi kwa Pita… Yote haya eti ni kwa niaba ya sheria… Kusema kweli, nina wasiwasi sana kuhusu kuishi katika nchi ambayo sheria na mahakama zinaweza kutumika kwa njia hii…”

Ujanja huu wa kisiasa kutoka mahakama kwa upande wa wasomi wanaounga mkono jeshi unaweza kuhatarisha utulivu wa nchi. Vijana wa Thailand waliompigia kura kwa wingi Pita na chama chake tayari wameahidi kuingia barabarani iwapo kura hiyo ya wananchi haitaheshimiwa.

Kwa sababu kiongozi huyo kijana, ambaye kwa hakika alifanikiwa kuunda muungano wa wengi wa vyama vinane, leo hii amezuiwa kwenye milango ya madaraka. Hata hivyo, alikuwa na nafasi ndogo sana ya kushinda kura ya ubunge, baada ya kushindwa mara ya kwanza. Alikosa kura za maseneta hamsini zaidi kati ya 250 - lakini maseneta wote ni watiifu kwa jeshi ambalo fanya uovu huo kwa kujificha.

Hali inayowezekana zaidi ni kwamba nguvu ya pili ya kisiasa katika muungano huu, Pheu Thai, inajaribu bahati yake na mgombea aliyekubaliwa zaidi, ambaye anaweza kuwa mfanyabiashara Srettha Thavisin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.