Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Thailand: Watoto 24 na watu wazima 11 wauawa na afisa wa zamani wa polisi

Akiwa na bunduki na kisu, mshambuliaji alianza mauaji yake katika shule ya chekechea ya Na Klang mchana katika mji wa Nongbua Lamphu, kaskazini mashariki mwa Thailand.

Mwanamke akilia mbele ya shule ya chekechea ya Na Klang baada ya shambulio lililogharimu maisha ya takriban watu 30, wakiwemo watoto.
Mwanamke akilia mbele ya shule ya chekechea ya Na Klang baada ya shambulio lililogharimu maisha ya takriban watu 30, wakiwemo watoto. © AP
Matangazo ya kibiashara

Afisa wa zamani wa polisi nchini Thailand amewaua watoto wasiopungua 24 na watu wazima 11 katika shambulio la bunduki na visu lililoanzia katika shule ya chekechea leo Alhamisi, duru rasmi zimesema. Kulingana na mamlaka, mshambuliaji alitoroka kituo cha kulelea watoto baada ya kutekeleza uhalifu wake, kisha akarudi nyumbani, ambapo alimuua mkewe na mtoto wao, kabla ya kujiua.

Picha na video za shule ya chekechea zilizotumwa mtandaoni zinaonyesha chumba kilichotapakaa damu sakafuni, magodoro yaliyotawanyika na vitambaa vikiwa vimening'inia ukutani.

Nje ya jengo hilo, wazazi waliokuwa wamefadhaika walitokwa na machozi.

Mamlaka imesema mauaji hayo yalitokea Alhamisi alasiri katika mji wa Nongbua Lamphu kaskazini mashariki mwa Thailand.

Jumla ya watoto 22 na watu wazima wawili waliuawa katika kituo cha kulea watoto kabla ya mshambuliaji kutoroka, kulingana na taarifa ya polisi. Lakini aliendelea kuwafyatulia risasi watu kutoka kwenye gari lake, Mkuu wa polisi Jenerali Paisal Luesomboon amesema. Polisi imesema pia mhalifu huyo aliwaua watoto wengine wawili na watu wazima tisa nje ya kituo cha kulelea watoto wadogo, akiwemo mkewe na mwanawe.

Vifo vinavyohusiana na bunduki nchini Thailand ni vidogo ikilinganishwa na vile vinavyotokea nchini Marekani na Brazili, lakini ni vya juu zaidi kuliko nchi kama vile Japani na Singapore ambazo zina sheria kali za udhibiti wa bunduki . Kiwango cha vifo vinavyohusiana na bunduki mnamo 2019 kilikuwa karibu vifo 4 kwa watu 100,000, ikilinganishwa na karibu vifo 11 kwa watu 100,000 nchini Marekani na karibu vifo 23 kwa watu 100,000 nchini Brazil.

Mwezi uliopita, mfanyakazi mmoja aliwapiga risasi wenzake katika Chuo cha kijeshi huko Bangkok, na kuua watu wawili na kumjeruhi mwingine kabla ya kukamatwa.

kisa kibaya zaidi cha mauaji ya watu wengi nchini humo ni kile cha mwanajeshi aliyekuwa na hasira na kufyatua risasi katika kituo cha biashara katika mji wa kaskazini-mashariki wa Nakhon Ratchasima mnamo 2020, na kuua watu 29 na kujaribu kuweka mbali vikosi vya usalama kwa takriban masaa 16 kabla ya kuuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.