Pata taarifa kuu
THAILAND-USALAMA

Shughuli za uokoaji zaendelea Thailand

Shughuli za uokoaji zimeanza tena leo Jumanne asubuhi nchini Thailand ili kuwaondoa vijana wanne wa mwisho na kocha wao wa soka waliokwama katika pango lililokumbwa na mafuriko kwa zaidi ya wiki mbili, mkuu wa kitengo cha dharura amesema.

Wavulana wanane waliokolewa kutoka kwenye pango lenye mafuriko kaskazini mwa Thailand walipokimbia zaidi ya wiki mbili zilizopita wako vizuri kiafya kwa ujumla, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Umma amesema.
Wavulana wanane waliokolewa kutoka kwenye pango lenye mafuriko kaskazini mwa Thailand walipokimbia zaidi ya wiki mbili zilizopita wako vizuri kiafya kwa ujumla, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Umma amesema. REUTERS/Athit Perawongmetha
Matangazo ya kibiashara

Waokoaji, kwa msaada wa wapiga mbizi, sasa wameweza kuondoa watu nane kati ya 13 waliobaki katika pango la Tham Luang, katika mkoa wa Chiang Rai, katika mazingira magumu, zoezi ambalo limetatizwa na.mvua zinazoendelea kunyesha.

Narongsak Osottanakorn amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa awamu ya mwisho ya uokoaji ilianza karibu saa 10:08 saa za Thailand (sawa na 01:08 saa za Afrika ya Kati).

"Tutaondoa watu watano kwa wakati mmoja," amesema. "Tunatarajia kwenda haraka leo," Narongsak Ossottanakorn ameongeza.

Waathirika nane wanaendelea vizuri," amesema Jumanne wiki hii Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Umma, Jesada Chokedamrongsuk.

Hata hivyo, Thongchai Lertwilairatanapong, Inspekta Mkuu wa Idara ya Afya, amesema kuwa vipimo vya damu vilivyofanywa kwa watoto hao vilionyesha kuwa wana "dalili za maambukizi."

Kundi la wavulana hao litawekwa chini ya uchunguzi katika hospitali kwa wiki moja, amesema.

Vijana walialikwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, katika fainali ya Kombe la Dunia itakayopigwa siku ya Jumapili huko Moscow, ikiwa watafanikiwa kuokolewa wote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.