Pata taarifa kuu

Thailand: Waziri Mkuu asimamishwa kazi na Mahakama ya Katiba, mgogoro wa kisiasa nchini

Hali ya kisiasa nchini Thailand yakumbwa na sintofahamu. Waziri Mkuu, Prayut Chan-ocha, amesimamishwa kazi mnamo Agosti 24 na Mahakama ya Kikatiba kwa sababu ya muda mrefu sana wa mamlaka yake: amefanya miaka minane madarakani.

Waziri Mkuu Prayut Chan-ocha amesimamishwa kazi na Mahakama ya Kikatiba. Itachukuwa uamuzi kuhusu mamlaka yake.
Waziri Mkuu Prayut Chan-ocha amesimamishwa kazi na Mahakama ya Kikatiba. Itachukuwa uamuzi kuhusu mamlaka yake. AP - Sakchai Lalit
Matangazo ya kibiashara

Hakuna angeliyeamini na Mahakama ya Kikatiba ya Thailand imeamua, kwa kura 4 kati ya 5, kusitisha mamlaka ya Waziri Mkuu Prayut Chan-ocha. Haya yote ni kwa ombi la upinzani, ambalo limeegemezwa kwenye ibara ya Katiba, yaani ukomo wa miaka minane ya muda wa juu wa mihula miwili inayowezekana ya Waziri Mkuu.

Madarakani hadi 2027?

Kiuhalisia, jenerali wa zamani wa jeshi Prayut Chan-ocha alitumia zaidi ya miaka minane mamlakani kwani ndiye aliyeanzisha mapinduzi ya Mei 2014 ambayo yaliiangusha serikali iliyochaguliwa. 

Mahakama sasa italazimika kuamua iwapo muhula wake ulianza rasmi kwa mapinduzi, kuanzishwa kwa serikali ya mpito, kupitishwa kwa Katiba mpya ya 2017 au uchaguzi mkuu wa 2019, ambapo hatimaye chama chake cha kisiasa kilishinda.

Ikiwa tafsiri hii ya mwisho itakubaliwa, inaweza kumruhusu Prayut Chan-ocha kusalia mamlakani hadi 2027, kwa masharti ya kuchaguliwa tena katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Machi ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.