Pata taarifa kuu
THAILAND

Bangkok: Waandamanaji elfu kadhaa waandamana kwa magari dhidi ya serikali

Waandamanaji elfu kadhaa wameandamana wakiwa ndani ya magari yao ili kuepusha misongamano na kukaribiana kutokana na janga la Corona huko Bangkok Jumapili hii wakidai kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Prayut Chan-O Cha, ambaye anaendelea kukosolewa kwa jinsi anavyoshughulikia mgogoro wa kiafya na athari zake kwa uchumi.

Mamia ya magari na pikipiki yalizuia barabara kuu zinazoingia katika mji mkuu wa Thailand wakati wa maamnadamano ya kupinga serikali
Mamia ya magari na pikipiki yalizuia barabara kuu zinazoingia katika mji mkuu wa Thailand wakati wa maamnadamano ya kupinga serikali Lillian SUWANRUMPHA AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya magari na pikipiki yalizuia barabara kuu zinazoingia katika mji mkuu wa Thailand, huku honi zikipigwa, wakati wapita njia wakikaribisha hatua hiyo kwa ishara ya vidole vitatu, ishara inayotumiwa na wapinzani wa serikali.

"Tunataka kujiuzulu mara moja kwa Prayut Chan-O-Cha. Yeye hana uwezo wa kusimamia nchi hii," amesema Nattawut Saikua, mwanasiasa ambaye alikuwa mshirika wa zamani wa karibu wa Waziri Mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra, hasimu mkuu wa serikali ya sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.