Pata taarifa kuu

China yazindua mazoezi ya kijeshi karibu na mpaka wa Myanmar

Beijing imeanza mazoezi ya kijeshi Jumamosi hii, Novemba 25 karibu na mpaka wa Myanmar. Luteka ya nguvu, wakati kwa mwezi mmoja, Myanmar imekuwa ikkumbwa mapigano makali kati ya utawala wa kijeshi na makundi ya waasi, katika mikoa iliyo karibu na China.

Mpaka kati ya China na Myanmar (Burma) huko Ruili, katika mkoa wa Yunnan magharibi.
Mpaka kati ya China na Myanmar (Burma) huko Ruili, katika mkoa wa Yunnan magharibi. AFP - NOEL CELIS
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Beijing, StΓ©phane Lagarde

Televisheni za China hazikuonyesha picha za mazoezi haya yanayoitwa "mapambano halisi". Na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka uongozi wa Jeshi la Ukombozi la Watu, iliyosomwa kwenye televisheni, haielezei muda wa operesheni, wala idadi ya askari au idadi ya vifaa vinavyotumiwa kwa mazoezi haya.

Mazoezi haya kwenye mpaka wa Myanmar ni sehemu ya mpango wa mafunzo wa kila mwaka kwa majeshi, taarifa inaeleza zaidi. Mazoezi haya yanakusudia kujaribu uwezo wa askari, kudhibiti na kufunga mpaka na kupeleka nguvu za mashambulizu kwa adui. Hiyo ni kwa ujumbe rasmi.

mazoezi haya makubwa yanafanyika siku moja baada ya kusonga mbele kwa waasi. Muungano wa waasi ulichukua udhibiti wa ngome kadhaa za jeshi na mji wa kimkakati ambapo biashara na China hupita.

Lengo la waasi ni kukata uhusiano kati ya China na serikali ya kijeshi, ambayo kwa hivyo inanyimwa ukwasi, hali ambayo imeilazimu Beijing kujibu. China ina nia ya kutetea maslahi yake ya kimkakati, ikiwa ni pamoja na maeneo ya gesi yanayoendeshwa na Wachina. Na ina wasiwasi juu ya kukosekana kwa utulivu pembezoni mwake.

Beijing imetoa wito kwa raia wake kuondoka "haraka iwezekanavyo" kutoka kwa mapigano ambayo yameongezeka kaskazini mwa Myanmar. Eneo lililo karibu na mpaka wa China, pia raia wa Myanmar wanatoroka kwa wingi ambao, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ni 80,000 ambao wametoroka makazi yao, jambo linalozua hofu ya wimbi jipya la wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.