Pata taarifa kuu
MYANMAR- SIASA.

Marekani imeitaka China kulaani kitendo cha Myanmar kuwanyonga wanaharakati

Marekani imetoa wito kwa China kuiekea Myanmar shinikizo zaidi kutokana na hatua  ya jeshi  nchini humo kuwanyonga wanaharakati wanne wa demokrasia.

 Ned Price -Msemaji wa mambo ya nje wa Marekani.
Ned Price -Msemaji wa mambo ya nje wa Marekani. AFP - NICHOLAS KAMM
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Washington Ned Price katika taarifa yake amesema kuwa China ndilo taifa peke ambalo linauwezo wa kuishawishi Myanmar zaidi kuliko nchi nyengine yoyote.

China kwa upande wake kupitia kwa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ametupilia mabali wito wa Marekani akisema kuwa China haina uwezo wa kuingilia mambo ya ndani ya mataifa mengine.

Kuhusu hatua ya Myanmar kuwanyonga wanaharakati wanne raia wa taifa hilo, Zhao Lijian amesema  Myanmar inapaswa kutumia sheria zake na katiba kusuluhisha tofauti zinazoikabili.

Ned Price vilevile ameyataka mataifa ya dunia kupiga marafuko uuzaji wa silaha za kijeshi kwa Myanmar. Washington iksema kuwa inawazia mbinu ya kuufungia utawala wa kijeshi nchini humo kutopata fedha.

Mwanaharakati Kyaw Min Yu, anayejuliakana zaidi kwa jina la Ko Jimmy, pamoja na mbunge wa zamani Phyo Zeya Thaw ni miongoni mwa walionyongwa na jeshi nchini humo.

Wanaharakati hao walikamatwa mwaka jana baada ya jeshi kuchukua madaraka wakituhumiwa kwa kujihusisha na vitendoi vya kigaidi.

Hukumu dhidi ya wanne hao imekashifiwa vikali na mashirika ya kiraia wanaosema kuwa kitendo hicho sio haki.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu katika umoja wa mataifa Michelle Bachelet ameeleza kusikitishwa kwake na hatua hiyo licha ya kuwepo kwa wito kwa jeshi kutowanyonga.

Mataifa ya umoja wa ulaya yakiwemo Australia, Canada, Japan, New Zealand, Norway, Korea kusini,Uingereza na Marekani nayo pia yamelaani kitendo hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.