Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Japan: Kishida afanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amefanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri leo Jumatano, hususa kwenye  wizara mbili muhimu, Mambo ya Nje na Ulinzi, na kuongeza idadi kubwa yaa wanawake katika serikali yake.

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida, ametangaza mawaziri ambao wamechukua nafasi za Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi, Yoshimasa Hayashi na Yasukazu Hamada mtawalia, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko makubwa ambayo pia yameongeza idadi ya wanawake katika timu ya serikali.
Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida, ametangaza mawaziri ambao wamechukua nafasi za Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi, Yoshimasa Hayashi na Yasukazu Hamada mtawalia, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko makubwa ambayo pia yameongeza idadi ya wanawake katika timu ya serikali. AP - Eugene Hoshiko
Matangazo ya kibiashara

Akiwa madarakani tangu Oktoba 2021, Bw. Kishida, 66, ameshuhudia umaarufu wake ukishuka katika miezi ya hivi karibuni, hali ambayo ilidhoofisha nafasi yake kama rais wa chama cha Liberal Democratic Party (PLD), chama cha kihafidhina cha mrengo wa kulia,  huku uchaguzi wa ndani ukipangwa kufanyika mwaka ujao.

Mabadiliko hayo yanalenga kufufua umaarufu wa waziri mkuu wa Japan miongoni mwa umma na msimamo wake ndani ya chama cha Liberal Democratic Party kabla ya uchaguzi wa mchujo mwaka ujao.

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida, ametangaza mawaziri ambao wamechukua nafasi za Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi, Yoshimasa Hayashi na Yasukazu Hamada mtawalia, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko makubwa ambayo pia yameongeza idadi ya wanawake katika timu ya serikali. Hayo yameripotiwa na idhaa ya umma ya "Nhk", ikibaini kwamba nafasi ya Hayashi imechukuliwa na aliyekuwa Waziri wa Sheria Yoko Kamikawa, 70, huku nafasi ya Hamada ikichukuliwa na Minoru Kihara, 54, aliyekuwa Katibu wa nayehusika na masuala ya Bunge.

Mabadiliko haya yanakuja katika hali ya mvutano mkali kati ya China na Korea Kaskazini. Idadi ya wanawake katika userikali itaongezeka kutoka wawili hadi watano. Waziri wa Fedha Shunichi Suzuki anatarajiwa ataendelea kushikilia wadhifa wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.