Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Japan: Waziri Mkuu Fumio Kishida anusurika kifo

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ameondolewa baada ya mlipuko uliofuatiwa na moshi kutokea alipokuwa akitoa hotuba katika Mkoa wa Wakayama (magharibi mwa Japani), vyombo vya habari vya ndani vimeripoti leo Jumamosi. 

Waziri Mkuu wa Japani Fumio Kishida akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Waziri Mkuu wa Japani Fumio Kishida akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari. AP - Efrem Lukatsky
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu yuko salama salimini, na mtu mmoja amekamatwa katika eneo la tukio, shirika la utangazaji la serikali NHK na vyombo vingine vya habari vya Japan vimeripoti.

Vyombo kadhaa vya habari, ikiwa ni pamoja na Shirika la Habari la Kyodo, vimeripoti kwamba kitu kinachofanana na "bomu la moshi" kilirushwa, lakini ilionekana kuwa hakuna majeraha au uharibifu ulioripotiwa katika eneo la tukio. Picha za televisheni zilionyesha umati wa watu ukihangaika, kisha mlio wa mlipuko ukifuatiwa na utoaji wa moshi mweupe.

Mtu mmoja amekamatwa katika eneo la tukio, katika bandari ya wavuvi ya Saikazaki katika mkoa wa Wakayama, ambapo Bw. Kishida alikuwa atoe hotuba ya uchaguzi, kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha umma cha NHK, ambacho kilirusha picha zinazomuonyesha mtu akiwa chini akiwa amezungukwa na wengine kadhaa. huku umati wa watu ukitawanyika. Mtu huyo amekamatwa kwa tuhuma za "kuzuia biashara", kulingana na kituo hicho. Hakuna uthibitisho rasmi uliotolewa mara moja na mamlaka, na polisi imekataa kutoa maoni.

Katika kampeni za uchaguzi

“Nilikuwa na mshtuko. Moyo wangu bado unadunda sana,” mwanamke mmoja katika eneo la tukio ameiambia NHK. Mtu mwingine ameambia kituo cha runinga kuwa hofu miongoni mwa umati ilianza hata kabla ya mlipuko huo, baada ya mtu kusema waliona kilipuzi kikirushwa.

Bw. Kishida alikuwa amemaliza kuonja samaki kwenye ukumbi huo na alikuwa anakaribia kuhutubia umati wa watu kumuunga mkono mgombea kutoka chama chake cha Liberal Democratic Party (LDP) katika uchaguzi mdogo ujao wa ubunge wa bunge hilo lilipotokea tukio hilo.

“Inasikitisha kwamba tukio la namna hii lilitokea katikati ya kampeni za uchaguzi, ambao ndio msingi wa demokrasia. Huu ni ukatili usiosameheka,” Hiroshi Moriyama, mkuu wa mikakati ya uchaguzi wa LDP, amekiiambia kituo cha NHK.

Usalama waimarishwa

Japan imeimarisha mipango yake ya usalama baada ya mauaji ya waziri mkuu wa zamani Shinzo Abe, ambaye alipigwa risasi na kuuawa alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya kampeni za uchaguzi mwezi Julai mwaka uliyopita. 

Aliyedaiwa kuhusika na muuaji wake, Tetsuya Yamagami, alisema alimlenga Bw. Abe kwa sababu ya madai yake ya uhusiano na dhehebu la Mwezi, ambalo pia linajulikana kama Kanisa la Muungano.

Tukio hili jipya linakuja wakati Japan ikiwa mwenyeji wa mikutano ya mawaziri ya G7 kaskazini na katikati mwa nchi mwishoni mwa wiki hii, na mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za kundi hili utafanyika mwezi Mei huko Hiroshima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.