Pata taarifa kuu
JAPAN- TANZIA

Shinzo Abe: Raia wa Japan wamemuomboleza waziri mkuu wao wa zamani.

Maelfu ya raia wamejitokeza katika barabara za jiji la Tokyo kutoa heshima zao za mwisho kwa waziri mkuu wa zamani Shinzo Abe.

Raia jijini Tokyo wakipiga foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa Shinzo Abe.
Raia jijini Tokyo wakipiga foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa Shinzo Abe. REUTERS - ISSEI KATO
Matangazo ya kibiashara

Gari lililokuwa limebeba mwili wake Abe limeonekana likipita katika baadhi ya barabara za jiji la Tokyo ambapo pia limesimama katika baadhi ya sehemu maalum  zilizotengwa kwa ajili ya kufanikisha  shughuli hiyo.

Awali, ibaada ya wafu ya Abe ilifanyika katika hekalu ya Zojoji ambapo watu wa familia yake pamoja na waombolezaji wachache walioruhusiwa kuhudhuria.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 67, aliuwawa kuwa kupigwa risasi siku Ijuma ya wiki iliyopita wakati akiwa katika shughuli za kampeni eneo la Nara kusini mwa Japan.

Milolongo mirefu ya waombolezaji wakiwa wamebeba maua imeokana katika jiji la Tokyo, bendera zikipeperushwa nusu mlingoti.

Wengi wa waombolezaji wametaja Abe kama mtu aliwahakikishia utulivu na usalama, baadhi wakimkumbuka kwa jinsi alivyo kabiliana na janaga la uviko 19 wakati akiwa waziri mkuu.

Msafara uliokuwa umbeba jeneza lake pia ulipita kando ya makao makuu ya chama chake Abe cha Liberal Democratic Party (LDP) kabla ya kuingia katika ofisi ya waziri mkuu ambapo ulipokelewa na waziri mkuu Fumio Kishida na viongozi wengine.

Msafara huo pia ulipita nje ya majengo ya bunge, eneo ambalo Abe aliingia kwa mara kwanza akiwa mbunge mnamo mwaka wa 1993.

Abe, ndiye waziri mkuu wa Japan aliyehudumu kwa muda mrefu ambapo ametajwa kama kiongozi aliyekuwa na ushawishi mkubwa nchini humo.

Polisi katika ripoti yake, inasema kuwa mtu aliyempiga risasi Abe alifanya hivyo kutokana na tofauti alizokuwa nazo na makundi ya kidini ambapo aliaamnini kuwa kiongozi huyo alikuwa miongoni mwa makundi hayo.

Mauwaji ya Abe, yalishutumiwa vikali na viongozi maarufu duniani, waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson akilaani kitendo hicho.

Rais wa Marekani Joe Biden alimpigia simu waziri mkuu wa Japan Kishida ambapo aliomboleza pamoja naye akitaja kitendo hicho kama janaga kwa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.