Pata taarifa kuu

G7 yakutana Hiroshima katikati ya vita nchini Ukraine na mzozo wa kiuchumi na China

Viongozi wa nchi saba zilizostawi zaidi kiviwanda, G7, wanakutana leo Ijumaa, Mei 19 katika mji wa Japan wa Hiroshima kwa mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo. Wanatarajia hasa, kujadili uimarishaji wa vikwazo dhidi ya Urusi na ulinzi dhidi ya "shurutisho la kiuchumi" kutoka China.

Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) akilakiwa na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida (kulia) kabla ya mkutano wao wa nchi mbili huko Hiroshima Mei 18, 2023, kabla ya Mkutano wa Viongozi wa G7.
Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) akilakiwa na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida (kulia) kabla ya mkutano wao wa nchi mbili huko Hiroshima Mei 18, 2023, kabla ya Mkutano wa Viongozi wa G7. AFP - KIYOSHI OTA
Matangazo ya kibiashara

Lengo la mkutano huu ni kuonyesha umoja dhidi ya Urusi na China. Kuanzia Ijumaa hadi Jumapili, ajenda ya majadiliano kati ya viongozi wa nchi wanachama wa G7 (Marekani, Japan, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Canada) itajiita kuhusu Ukraine. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kushiriki katika mkutano huo kwa njia ya video na "majadiliano kuhusu hali kwenye uwanja wa vita" yanatarajiwa, amesema Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan.

Kulingana afusa huyu, suala la kuimarishwa kwa vikwazo dhidi ya Urusi linapaswa pia kushughulikiwa na nchi wanachama. Jake Sullivan amesema viongozi hao watajadili kuhusu kukabiliana na msukosuko wa vikwazo, ambao unamruhusu Rais wa Urusi Vladimir Putin kuendelea kufadhili juhudi zake za vita.

Nyuklia

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida akiwakaribisha wageni wake mjini Hiroshima. Mnamo Agosti 6, 1945, jiji hilo liliharibiwa na bomu la atomiki la Marekani na kusababisha watu 140,000 kuangamia. Pia anakusudia kuchukua fursa hii kujadili upunguzaji wa silaha za nyuklia. Fumio Kishida, ambaye familia yake inatoka Hiroshima na ambaye yeye mwenyewe alichaguliwa huko, kwa hiyo anataka kuwatia moyo wageni wake, hasa Uingereza, Ufaransa na Marekani, nchi ambazo kwa pamoja zinamiliki maelfu ya vichwa vya nyuklia, kujitolea kuwa wazi kuhusu hifadhi zao na kupunguza silaha zao.

Hata hivyo, matumaini ya maendeleo katika eneo hili ni madogo kutokana na kuongezeka kwa mvutano kati ya Urusi, Korea Kaskazini na China, mataifa mengine yenye nguvu za nyuklia. Kwa upande wa Urusi, kumekuwa na matamko mengi ya kutishia matumizi ya silaha za nyuklia.

'Sio G7 inayopinga China'

Kuhusiana na suala la uchumi, ni kwenye faili la China ambapo nchi za G7 zitalazimika kukubaliana, na hasa juu ya jinsi ya kujilinda kutokana na uhujumu wa kiuchumi unaowezekana kutoka kwa Beijing. Kwa mujibu wa mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan, viongozi wa G7 wanapaswa kukemea "shurutisho hili la kiuchumi" na kujitahidi kuondokana na tofauti za kupita Atlantiki kuhusu msimamo wa kupitisha China.

Lakini kwa nchi nyingi za Ulaya, hasa Ufaransa na Ujerumani, kuondoa hatari haimaanishi kukata uhusiano na China, mojawapo ya soko kubwa zaidi duniani. "Sio kundi la G7 dhidi linalopinga China", iesisitiza Ikulu ya Elysée kabla ya mkutano huo, ikitamani "ujumbe chanya" wa ushirikiano "mradi tu kujadili pamoja". Nchi nane, zikiwemo India na Brazil, pia zimealikwa. Lengo ni kuwakusanya baadhi ya viongozi hao kupinga vita vya Ukraine na matarajio ya Beijing.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.