Pata taarifa kuu

Pyongyang: Mwanajeshi wa Marekani atoroka jeshi kutokana na ubaguzi wa rangi

Mwanajeshi wa Marekani aliyehamia Korea Kaskazini mwezi Julai alitaka kuepuka "kutendewa vibaya na ubaguzi wa rangi katika jeshi la Marekani", shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limesema leo Jumatano, uthibitisho wa kwanza rasmi wa kuzuiliwa kwa Travis King na Pyongyang.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali vya Korea Kaskazini, mwanajeshi wa Marekani Travis King alikiri "kuingia kinyume cha sheria" nchini Korea Kaskazini Julai 18 na kueleza nia yake ya kupata hifadhi nchini humo au katika nchi ya tatu.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali vya Korea Kaskazini, mwanajeshi wa Marekani Travis King alikiri "kuingia kinyume cha sheria" nchini Korea Kaskazini Julai 18 na kueleza nia yake ya kupata hifadhi nchini humo au katika nchi ya tatu. © Ahn Young-joon, AP
Matangazo ya kibiashara

"Kulingana na uchunguzi wa chombo husika cha DPRK (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea), Travis King amekiri kuingia katika eneo la DPRK kinyume cha sheria," KCNA imeripoti, ikitumia jina rasmi la Korea Kaskazini.

Hii ni taarifa ya kwanza kwa umma ya Pyongyang tangu kuanza kwa kesi ya King. Mwanajeshi huyu wa Marekani alitakiwa kurejea Marekani baada ya kupata matatizo na vyombo vya sheria vya Korea Kusini, lakini kwa alivuka mpaka na kuingia Korea Kaskazini Julai 18 huku akijumuika na kundi la watalii waliotembelea eneo lisilo la kijeshi linalotenganisha Korea mbili.

"Wakati wa uchunguzi, Travis King alisema aliamua kuja DPRK kwa sababu alipinga unyanyasaji wa kinyama na ubaguzi wa rangi katika jeshi la Marekani," KCNA imesema.

- 'Awekwa chini ya udhibiti' -

Travis King "aliwekwa chini ya udhibiti na wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Korea alipoingia kimakusudi" eneo la Korea Kaskazini, shirika hilo lahabari limeongeza, na kuthibitisha kuzuiliwa kwa mwanajeshi wa Marekani kwa mara ya kwanza.

Bw. King "alionyesha nia yake ya kutafuta kimbilio katika DPRK au katika nchi ya tatu, akisema amekatishwa tamaa na jamii ya Marekani isiyo na usawa", ameihakikishia KCNA, ikibainisha kuwa uchunguzi wa serikali bado unaendelea.

Travis King aliachiliwa kutoka jela nchini Korea Kusini baada ya rabsha katika baa na ugomvi na polisi. Ilibidi arejee Marekani kukabiliana na vikwazo vya kinidhamu.

Siku ya Alhamisi Agosti 3, kamandi ya Marekani ilisema kwamba Pyongyang "ilijibu" maombi kuhusu askari huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.