Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini yarusha makombora mawili ya balestiki

Korea Kaskazini imerusha makombora mawili ya masafa mafupi siku ya Jumanne, Seoul imetangaza siku moja baada ya kuanza kwa luteka kubwa zaidi ya pamoja na Marekani katika kipindi cha miaka mitano.

Korea Kaskazini imerusha makombora mawili ya masafa mafupi, kulingana na jeshi la Korea Kusini.
Korea Kaskazini imerusha makombora mawili ya masafa mafupi, kulingana na jeshi la Korea Kusini. Jung Yeon-je / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Jeshi letu limegundua makombora mawili ya masafa mafupi yaliyorushwa (...) kati ya 07:41 na 07:51" ambayo yaliruka umbali wa takriban kilomita 620, Wakuu wa Majeshi wamesema katika taarifa. "Majeshi yetu yameimarisha ukaguzi na umakini kwa kutarajia uzinduzi mwingine, huku yakisimama tayari kuingilia kati katika mfumo wa ushirikiano wa karibu kati ya Korea Kusini na Marekani," Seoul imeongeza.

Msemaji wa serikali ya Japan Hirokazu Matsuno amesema kuwa makombora hayo hayakutua katika maji ya Japan. Tokyo inashuku Korea Kaskazini kwa kutaka kujihusisha na "chokochoko mpya".

Siku ya Jumapili, Pyongyang ilirusha makombora mawili kutoka manowari, katika mkesha wa kuanza kwa mazoezi ya pamoja kati ya Seoul na Washington yaliyopewa jina la "Freedom Shield", ambayo yanapaswa kudumu angalau siku kumi na kuzingatia "mageuzi ya "mazingira ya usalama" kutokana na uchokozi ulioongezeka maradufu wa Korea Kaskazini, washirika hao walisema.

Pyongyang ilidai kuwa uzinduzi huo ulilenga kujaribu "vizuizi vyake vya nyuklia katika maeneo tofauti", huku ikikosoa mazoezi kati ya washirika hao wawili.

Aina hii ya mazoezi, iliyokusudiwa kulingana na washirika hao wawili kupigana dhidi ya vitisho vinavyoongezeka kutoka Pyongyang, huamsha hasira ya Korea Kaskazini. Pyongyang inayaona kama mazoezi yenye lengo la kuivamia ardhi yake na mara kwa mara huahidi hatua "kali" katika kukabiliana na mazoezi hayo.

Jeshi la Korea Kusini lilisema kuwa mazoezi hayo yatahusisha "taratibu za wakati wa vita ili kuzima mashambulizi ya Korea Kaskazini na kufanya kampeni ya kuleta utulivu Kaskazini."

'Maonyesho mapya ya Nguvu'

Mnamo mwaka 2022, Pyongyang iliita hadhi yake kama nguvu ya nyuklia "isiyoweza kutenduliwa" na ilifanya rekodi ya majaribio ya balestiki kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wiki iliyopita, kiongozi Kim Jong Un aliagiza jeshi lake kuongeza maazoezi ya kijeshi kwa "vita vya kweli". Iwapo Pyongyang itahalalisha majaribio yake ya makombora kwa kunyooshea kidole mazoezi ya kijeshi Kusini, pia itatimiza lengo la kitaifa, anasema Leif-Eric Easley, profesa katika Chuo Kikuu cha Ewha huko Seoul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.