Pata taarifa kuu
ULINZI-DIPLOMASIA

Pyongyang: Hali kwenye rasi ya Korea iko kwenye 'kikomo cha mwisho cha mstari mwekundu'

Mazoezi ya kijeshi pamoja kati ya Korea Kusini na Marekani yamefanya hali kuwa "kikomo kikubwa cha mstari mwekundu". Taarifa iliyotiwa saini na Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini, Alhamisi, Februari 2, ambayo ni jibu la moja kwa moja kwa maoni yaliyotolewa na mkuu wa Pentagon, akisafiri kwenda Seoul mapema wiki hii. Afisa huyuo alitaja, pamoja na mambo mengine, kuimarika kwa mazoezi ya kijeshi na uigaji wa majibu ya nyuklia kwa matumizi ya Pyongyang ya bomu la atomiki.

Vifaru chapa K-9 vya Korea Kusini vikiwa kwenye mazoezi karibu na mpaka wa Korea mbili.
Vifaru chapa K-9 vya Korea Kusini vikiwa kwenye mazoezi karibu na mpaka wa Korea mbili. AP - Ahn Young-joon
Matangazo ya kibiashara

Akija Korea Kusini kumhakikishia mshirika wake uungwaji mkono wa Marekani, Lloyd Austin, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, kwa vyovyote vile, atafanikiwa kupata majibu kutoka Korea Kaskazini. Pyongyang inasema haina nia ya kufanya mazungumzo, mradi tu Washington inaendelea na "sera yake ya uhasama".

Upanuzi wa mazoezi

Ikiwa Ikulu ya White House imerejesha mwaliko wake wa mazungumzo, mkutano wa Jumanne kati ya mawaziri wa ulinzi wa Marekani na Korea Kusini ulithibitisha mkakati shambulizi wa nchi hizo mbili. Upanuzi wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi, kupelekwa kwa njia mpya za kimkakati na uthibitisho wa kufanyika mazoezi ya kuiga kwa matumizi ya silaha za nyuklia mnamo mwezi Februari. Washirika hao wawili pia walirusha ndege za kivita Jumatano hii, Februari 1.

Tishio la moja kwa moja

Vitendo na maneno mengi yanayolenga kushawishi maoni ya umma na sehemu ya wanasiasa la uthabiti wa muungano kati ya Seoul na Washington, wakati wazo la mpango wa nyuklia wa Korea Kusini linazidi kuwa maarufu. Lakini kaskazini mwa sambamba ya 38, yote haya yanaonekana kama tishio la moja kwa moja. Pyongyang inahakikisha kwamba "mazoezi haya ya kijeshi ya makabiliano na vitendo vya uhasama" vinaweza kubadilisha rasi ya Korea kuwa "eneo muhimu zaidi la vita".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.