Pata taarifa kuu
Korea Kaskazini- Marekani-Korea Kusini

Marekani na Korea Kusini kujibu Korea Kaskazini kuhusu nyukilia

Marekani na Korea Kusini, zinapanga kujibu ipasavyo hatua yoyote ya utawala wa Korea kaskazini kuamua kutumia silaha za nyuklia, wakati huu rais Joe Biden, akisema kikosi kazi kilichoundwa kinatathmini hatua za kuchukua.

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Korea Kusini  Yoon Suk-yeol
Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Matamshi ya Marekani yamekuja wakati huu hofu ya Korea Kaskazini kutumia silaha za nyuklia ikiongezeka kwenye eneo la ukanda.

Karine Jean-Pierre, ni msemaji wa ikulu ya Marekani, White House.

Baada ya kikao cha Cambodia rais Biden na Yoon waliagiza kikosi walichokiunda kufanya tathimini ya hatua za kuchukua hata pale ambapo Korea kaskazini itatumia nyukilia. Ameeleza Jean- Pierre. 

Rais wa Korea Kaskazini katika siku za karibuni ameonekana kumaimarisha mazoezi ya silaha zake la nyukilia, hatua ambayo imekashifiwa vikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.