Pata taarifa kuu

Yonhap: Korea Kaskazini imerusha kombora la balestiki

Korea Kaskazini imerusha kombora la balestiki siku ya Jumapili, kulingana na shirika la habari la Yonhap, uzinduzi wa hivi punde zaidi wakati Seoul na Washington zikifanya mazoezi yao makubwa zaidi ya kijeshi katika kipindi cha miaka mitano.

Mwaka jana, Korea Kaskazini ilitangaza hadhi yake kama nguvu ya nyuklia "isiyoweza kutenduliwa", huku kiongozi wake Kim Jong-un akitoa wito wa kuongezwa "kwa kasi" kwa silaha zake za kijeshi, ikiwa ni pamoja na silaha za kiteknolojia za nyuklia.
Mwaka jana, Korea Kaskazini ilitangaza hadhi yake kama nguvu ya nyuklia "isiyoweza kutenduliwa", huku kiongozi wake Kim Jong-un akitoa wito wa kuongezwa "kwa kasi" kwa silaha zake za kijeshi, ikiwa ni pamoja na silaha za kiteknolojia za nyuklia. AP
Matangazo ya kibiashara

"Korea Kaskazini inarusha kombora la balestiki kuelekea Bahari ya Mashariki," imesema makao makuu ya majeshi huko Seoul, ikinukuliwa na shirika la habari la Yonhap, ikimaanisha korea Kaskazini kuelekea Bahari ya Japan.

Seoul imekuwa ikifanya mazoezi ya kijeshi na Washington tangu siku ya Jumatatu, ambayo hayajawahi kufanywa katika miaka mitano, lengo ikiwa ni kuimarisha ushirikiano wa washirika hao wawili katika kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka Kaskazini. Mazoezi hayo yanayoitwa "Freedom Shield" (Ngao ya Uhuru), yatadumu kwa siku kumi.

Mazoezi haya yanaikasirisha Pyongyang, ambayo huyaona kama mazoezi ya uvamizi wa ardhi yake na mara kwa mara huahidi majibu "mzito".

Uzinduzi huo unakuja baada ya Pyongyang kurusha kombora lake lenye nguvu zaidi, Hwasong-17 intercontinental ballistic missile (ICBM), siku ya Alhamisi kabla ya ziara ya Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol nchini Japan.

Majirani hao wawili wameimarisa ngome yao katika kiwango cha juu na kuamua kutangaza msimamo mmoja dhidi ya uchokozi wa Korea Kaskazini.

Lilikuwa ni jaribio la pili la ICBM kufanywa na Pyongyang mwaka huu.

Vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini vimesema kuwa ni jibu kwa mazoezi ya kijeshi "ya kutisha" ya Korea Kusini na Marekani.

Mwaka jana, Korea Kaskazini ilitangaza hadhi yake kama nguvu ya nyuklia "isiyoweza kutenduliwa", huku kiongozi wake Kim Jong-un akitoa wito wa kuongezwa "kwa kasi" kwa silaha zake za kijeshi, ikiwa ni pamoja na silaha za kiteknolojia za nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.