Pata taarifa kuu

India yapiga marufuku usafirishaji wa mchele mweupe usio wa Basmati

Serikali ya India ilitangaza Alhamisi, Julai 20 kupiga marufuku uuzaji wa mchele mweupe usio wa basmati nje ya nchi, kwa lengo la kuzuia mfumuko wa bei wa bidhaa hii muhimu, ambayo nchi hiyo ni muuzaji wa kwanza duniani. Bei ya mchele imepanda kwa kasi katika soko la ndani katika wiki za hivi karibuni.

Mkulima wa Kihindi akivuna mpunga katika shamba moja nje ya Guwahati mnamo Juni 6, 2023. India ndiyo msafirishaji mkuu wa bidhaa hiyo duniani.
Mkulima wa Kihindi akivuna mpunga katika shamba moja nje ya Guwahati mnamo Juni 6, 2023. India ndiyo msafirishaji mkuu wa bidhaa hiyo duniani. © Anupam Nath / AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko New Delhi, Sébastien Farcis

Bei ya mchele imepanda kwa 3% katika mwezi mmoja nchini India, na 11% kwa mwaka, na mtazamo wa miezi ijayo sio mzuri: mafuriko ya hivi karibuni kaskazini mwa nchi yamekumba mashamba yaliyopandwa hivi karibuni ya Punjab, mojawapo ya maghala ya mpunga, na itakuwa muhimu kupanda upya haraka ili kuokoa msimu wa kilimo wa mchele huo. Mfumo wa hali ya hewa unaojulikana kama El Nino pia utaleta mvua kidogo katika miezi ijayo.

New Delhi inataka kuzuia hatari ya uhaba na mfumuko wa bei ya chakula, hasa miezi 10 kabla ya uchaguzi wa wabunge: kwa hivyo mamlaka imepiga marufuku usafirishaji wowote wa mchele mweupe usio wa Basmati. Hii inaondoa 45% ya mauzo ya muuzaji mkuu wa mchele kwenye soko.

Barani Afrika, nchi za kwanza kuathirika zitakuwa Senegal, Côte d'Ivoire, Benin na Togo, ambao ni wateja wakuu wa India: Watalazimika kugeukia Thailand na Vietnam. Lakini bei zao zinapaswa kuongezeka haraka: mchele uliovunjika wa Kivietinam ulipanda bei wiki hii tangu miaka 12 iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.