Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

India: Watu kadhaa wauawa na wengine kujeruhiwa katika ghasia za uchaguzi

Takriban watu saba wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa siku ya Jumamosi nchini India katika makabiliano yaliyohusishwa na uchaguzi wa srikali za mitaa huko West Bengal, eneo linalokumbwa na ghasia za mara kwa mara za kisiasa wakati wa kampeni za uchaguzi.

Wafuasi wa chama cha Kihindu cha BJP wakati wa mkutano wa uchaguzi huko Calcutta, West Bengal, Aprili 5, 2021.
Wafuasi wa chama cha Kihindu cha BJP wakati wa mkutano wa uchaguzi huko Calcutta, West Bengal, Aprili 5, 2021. AP - Bikas Das
Matangazo ya kibiashara

Chama tawala nchini India cha Bharatiya Janata Party (BJP) kimeongeza juhudi zake katika miaka ya hivi karibuni kupata nafasi katika Bengal Magharibi - inayotawaliwa na chama cha kikomunisti kwa sehemu kubwa ya historia yake - ili kupanua wigo wa kisiasa kwa chama hicho katika eneo hilo.

Wapiga kura wamepiga kura zao Jumamosi huku kukiwa na mvutano mkubwa wa uchaguzi wa kuteua maafisa wa manispaa kutoka miongoni mwa wagombea zaidi ya 200,000 kote Bengal Magharibi, jimbo lenye wakazi zaidi ya milioni 104.

"Watu saba wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika ghasia zinazohusiana na uchaguzi katika vijiji tofauti jimboni humo," Jawed Shamim, afisa mkuu wa polisi wa Bengal Magharibi kaskazini-mashariki mwa Bangladesh, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kanda za video zilizorushwa na vyombo vya habari nchini zinaonyesha wafanyakazi wa vyama pinzani wakizurura mitaani na virungu, pamoja na masanduku ya kura yaking'olewa na kuchomwa moto nje ya vituo vya kupigia kura. Idadi kubwa ya vikosi vya usalama iliwekwa mbele ya ofisi zingine.

Zaidi ya mabomu 200 yaliyotengenzwa kienyeji - ambayo yalitumika mara kwa mara wakati wa uchaguzi huko West Bengal na kuuzwa kwa bei nafuu katika soko magendo ili kuwatisha wapiga kura - pia yalikamatwa wakati wa uchaguzi, polisi imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.