Pata taarifa kuu
USALAMA-AJALi

Karibu watu 300 wafariki katika mojawapo ya ajali mbaya zaidi ya reli nchini India

Takriban watu 288 wameuawa na zaidi ya 900 kujeruhiwa katika ajali ya reli iliyohusisha treni kadhaa mashariki mwa India, afisa mkuu wa eneo hilo alitangaza Ijumaa Juni 2. Ingawa shughuli za uokoaji kwenye eneo hilo sasa zimekamilika, idadi kubwa ya waathiriwa bado wanahudumiwa katika hospitali za jimbo hilo.

Waokoaji wako katika eneo la ajali ya treni nchini India mnamo Juni 3, 2023.
Waokoaji wako katika eneo la ajali ya treni nchini India mnamo Juni 3, 2023. AFP - DIBYANGSHU SARKAR
Matangazo ya kibiashara

"Operesheni ya uokoaji imekwisha," afisa wa idara ya uratibu wa dharura huko Balasore, karibu na eneo la mkasa, ameliambia shirika la habari la AFP. "Miili yote na abiria waliojeruhiwa wameondolewa kwenye eneo la ajali. "

Ajali hiyo ilitokea katika jimbo la Odisha, mashariki mwa India. Idadi ya vifo kufikia sasa imefikia 288. Treni ya abiria ambayo ilikuwa imetoka tu kuelekea kusini mwa Calcutta, Coromandel Express, na treni ya mizigo ziligongana karibu na Balasore, takriban kilomita 200 kutoka Bhubaneswar, mji mkuu wa jimbo hilo, mashahidi na wasemaji wa mamlaka za kikanda wamesema.

Treni ya pili ya abiria, iliyowasili kutoka kusini, pia ilihusika katika mkasa huo, kulingana na Pradeep Jena, afisa mkuu wa serikali katika jimbo hilo, lakini hali halisi ambayo ilitokea bado haijulikani.

'Nilijikuta na watu kadhaa juu yangu'

Mwanamume aliyeokolewa katikati ya usiku anashuhudia ajali hiyo kwenye kituo cha habari cha nchini India. “Nilikuwa nimelala niliposikia mshtuko wa ajali. Na niliishia na watu kama kumi juu yangu. Nilijeruhiwa mkononi na kichwani. Kisha nikaona watu karibu nami. Wengine walikuwa wamepoteza mikono, wengine miguu,” anasema.

Kwa ujumla, mabehewa kadhaa, yenye mamia ya abiria, yalilala chini na mengine kupitana, juu anaripoti mwandishi wetu wa New Delhi, Sébastien Farcis.

Narendra Modi azuru eneo la ajali

Saa chache baada ya janga hilo, mamlaka ya kikanda na shirikisho ilipeleka zaidi ya magari 200 ya wagonjwa, pamoja na timu kadhaa za uokoaji.

"Tumetayarisha hospitali zote kuu za umma na za kibinafsi, kutoka eneo la ajali hadi mji mkuu wa jimbo, kutunza majeruhi," amesema SK Panda, msemaji wa mamlaka ya Jimbo.

Katika hospitali za mikoa, makumi ya miili ya marehemu imetawanywa sakafuni, ikiwa imefunikwa kwa shuka nyeupe, ili kutambuliwa na familia. Na mamia ya walionusurika wanatibiwa, wamelazwa kwenye machela, au wameketi chini kwenye barabara za ukumbi zilizojaa watu. 

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amezuru eneo la ajali kwa helikopta. “Mawazo yangu yako kwa familia zilizofiwa. Na waliojeruhiwa wapone haraka,” Bw Modi ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, akiongeza kwamba alikuwa amezungumza na Waziri wa Shirika la Reli Ashwini Vaishnaw kutoa “taarifa halisi kuhusu hali hiyo”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.