Pata taarifa kuu
INDIA-JAMII

India: wakulima wavunja kambi yao baada ya mwaka mmoja wa maandamano

Maelfu ya wakulima wa India walikuwa wakipakia mali zao na kubomoa kambi iliyokuwa imejengwa kwa mahema viungani mwa New Delhi siku ya Jumamosi ili kurejea nyumbani baada ya mwaka mmoja wa maandamano dhidi ya sera za kilimo za serikali.

Wakulima wa India wakibomoa vibanda walivyojenga kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita huko Ghazipur, kitongoji cha New Delhi.
Wakulima wa India wakibomoa vibanda walivyojenga kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita huko Ghazipur, kitongoji cha New Delhi. AP - Altaf Qadri
Matangazo ya kibiashara

Mamia yao walikuwa wakicheza na kusherehekea "ushindi" Jumamosi asubuhi huku wakiondoa vizuizi barabarani na kubomoa vibanda vya kujihifadhi kwenye barabara kuu.

Waziri Mkuu Narendra Modi aliiomba bunge mwezi uliopita kufuta sheria tatu za mageuzi ya ardhi ambazo waandamanaji walisema zingeruhusu makampuni ya kibinafsi kudhibiti sekta ya kilimo nchini humo.

Hata hivyo, waandamanaji hao awali walikataa kuondoka kwenye kambi zao, wakitoa madai mengine, kama vile hakikisho la bei ya chini kabisa ya bidhaa zao za kilimo.

Serikali imeahidi kuunda tume kuhusu suala hilo na imeahidi kusitisha mashtaka ya wakulima wanaochoma mabua ya mazao, wanaotuhumiwa kuchafua hali ya hewa mjini New Delhi kila msimu wa baridi.

Mamlaka pia ilikubali kulipa fidia kwa familia za mamia ya wakulima ambao wanasema walikufa wakati wa maandamano na kusimamishwa kwa kesi ya jinai dhidi ya waandamanaji.

"Tulidhamiria kuandamana kwa muda mrefu iwezekanavyo. Lakini sote tuna furaha kwamba serikali ilikubali madai yetu na kwamba tumeweza kurejea nyumbani," Sativinder Singh, mmoja wa waandamanaji, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Ni siku nzuri kwa wakulima kwa sababu tunaweza kurejea kwa amani majumbani mwetu," ameongeza.

"Serikali sasa italazimika kutimiza ahadi zilizotolewa kwetu," Baljot Bawja, muandamanaji mwingine, ameliambia shirika la habaria la AFP.

“Hatuna nia ya kurejea mitaani, lakini ikiwa Serikali itakataa kutekeleza ahadi zake, hatutasita kufanya hivyo,” ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.