Pata taarifa kuu

India: Bunge labatilisha mageuzi ya kilimo ya Modi baada ya serikali kubatilisha

Bunge la India limerasimisha uondoaji wa sheria tatu za kilimo zenye utata. sheria hizo zilisababisha makumi ya maelfu ya wakulima kupiga kambi karibu na New Delhi kwa mwaka mmoja kupinga mageuzi haya katika sekta hiyo, kwa hofu kwamba mapato yao yatashuka na kuwasili kwa makampuni ya biashara ya kilimo.

Wafuasi wa upinzani nchini India, katika mkutano wa kutaka kufutwa kwa sheria tatu za kilimo ambazo zimesababisha maandamano ya kiraia kwa mwaka mmoja, huko New Delhi, Novemba 29, 2021.
Wafuasi wa upinzani nchini India, katika mkutano wa kutaka kufutwa kwa sheria tatu za kilimo ambazo zimesababisha maandamano ya kiraia kwa mwaka mmoja, huko New Delhi, Novemba 29, 2021. © AP - Manish Swarup
Matangazo ya kibiashara

Baada ya hali hii, upinzani unaibuka ukiwa na nguvu na kuongeza shinikizo kwa serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi.

Ilichukua dakika chache kwa Mabunge yote mawili kubatilisha sheria tatu za mashamba ambazo zimesumbua nchi kwa zaidi ya mwaka mmoja. Utaratibu huo ulikuwa wa haraka, kama vile kupitishwa kwa sheria hizi mwezi Septemba 2020 : chama cha wengi kilikataa uchunguzi wao na kamati ya bunge.

Upinzani unaidhinisha uondoaji huu, lakini unashutumu njia isiyo ya kidemokrasia ya kufanya hivyo. Rahul Gandhi ni Mbunge kutoka Chama cha Congress: "Sheria hizi tatu zilionyesha kwamba kulikuwa na nguvu nyuma ya Waziri Mkuu na maamuzi yake, na tulitaka kuzungumza juu ya hili Bungeni. Tulitaka pia kujadili sheria ya bei ya chini ya ununuzi wa bidhaa za kilimo na wakulima 700 waliokufa wakati wa maandamano. Lakini hatukuruhusiwa kufanya hivyo, na inaonyesha ni jinsi gani serikali inaogopa kuzungumzia lolote kati ya haya. "

Serikali inashikilia kuwa, kwa vile upinzani ulitaka sheria hizi ziondolewe, hakukuwa na haja ya kuwa na majadiliano.

Wakulima wengi sasa wanaweza kuondoka kwenye maeneo ya maandamano karibu na New Delhi, lakini kiongozi mashuhuri wa chama cha wakulima anatoa wito kwa mapambano kuendelea kwa sheria hii ya bei ya chini ya ununuzi katika kilimo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.