Pata taarifa kuu
INDIA-MAJANGA

India: Takriban watu 30 wafariki au kutoweka katika mafuriko

Takriban watu 30 wamefariki au kupotea kufuatia mafuriko yaliyotokea kusini mwa India, vyombo vya habari vimeripoti Jumamosi hii, huku vikibaini kwamba mabasi matatu yamesombwa na maji

Takriban watu 42 waliuawa mwezi uliopita wakati mvua kubwa iliyonyesha Kerala.
Takriban watu 42 waliuawa mwezi uliopita wakati mvua kubwa iliyonyesha Kerala. REUTERS/Indian Air Force
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi wa idara ya uokoaji wametoa miili mingi baada ya mabasi matatu kusombwa na maji katika jimbo la pwani la Andhra Pradesh siku ya Ijumaa.

Takriban watu wengine 18 bado hawajulikani walipo, kulingana na tovuti ya habari ya The NewsMinute.

Hali ya hewa isiyotabirika ambayo imekumba eneo la kusini mwa Asia katika miaka ya hivi karibuni inasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na hasa ukataji miti, ujenzi wa mabwawa na maendeleo kupita kiasi, wataalam wanasema.

Makumi ya watu wamekufa tangu mwezi Oktoba nchini India kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa, na wataalamu wa hali ya hewa wameripoti mvua kubwa katika maeneo kadhaa ya kusini Jumamosi.

Takriban watu 42 waliuawa mwezi uliopita wakati mvua kubwa iliyonyesha Kerala.

Siku ya Ijumaa, mamlaka ilipiga marufuku kuingia katika kanisa la Sabarimala, mojawapo ya madhabahu takatifu zaidi ya Uhindu, kutokana na mvua kubwa.

Tangu wiki iliyopita, mamia ya waumini wanakuja Sabarimala kila siku kama sehemu ya hija ya kila mwaka ambayo huchukua miezi miwili.

Kuongezeka kwa maji ya Mto wa Pamba kulilazimisha mamlaka kupiga marufuku waumini kwenda huko kwa siku moja, gazeti la Hindustan Times limeripoti Jumamosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.