Pata taarifa kuu

Lukashenko asema alimwambia Putin asimuue mkuu wa Wagner

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema siku ya Jumanne kwamba alimwambia Vladimir Putin asimuue bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin wakati wa uasi wake wa kutumia silaha ambao ulisitishwa. Lukashenko ambaye ni mshirika wa karibu wa Moscow, alichukua nafasi ya mpatanishi katika mzozo huo, akimpokea Yevgeny Prigozhin na watu wake ambao wanataka hivyo ndani ya mfumo wa makubaliano yaliyofanywa naye.

Picha iliyochapishwa Jumanne, Juni 27, 2023 na ofisi ya waandishi wa habari ya rais Alexander Lukashenko, huko Minsk.
Picha iliyochapishwa Jumanne, Juni 27, 2023 na ofisi ya waandishi wa habari ya rais Alexander Lukashenko, huko Minsk. AP
Matangazo ya kibiashara

"Nilimwambia Putin: tunaweza kumuua, sio shida. Ama kwa jaribio la kwanza au la pili. Lakini nilisema: usifanye hivyo, "amesema Alexander Lukashenko mbele ya maafisa wa Belarus, kulingana na video iliyorushwa hewani na kituo cha Telegram chenye uhusiano wa karibu na ofisi ya rais, Pool Pervogo. Rais wa Belarus pia ameeleza katika video hii kuwa alikuwa na Yevgeny Prigozhin amesema aliongea kwa simu mara saba na Yevgeny Prigozhin alipoanziha uasi dhidi ya Moscow, pamoja na mara sita kwa ombi la mkuu wa Wagner. Pia, amesema, alijaribu kuwahakikishia Wabelarus wasiwasi kuhusu kuwasili kwa mamluki hawa kwenye ardhi yao. “Kama makamanda wao watakuja kwetu na kutusaidia… Huo ni uzoefu. Wako mstari wa mbele, ni vitengo vya mashambulizi. Watatufafanulia mambo muhimu ya kijeshi kwa sasa”.

Taarifa za Alexander Lukashenko ambazo zinakuja wakati vyombo vya habari kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ukraina Pravda, vimebaini kwamba kiongozi wa kundi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, amewasili Minsk, mji mkuu wa Belarus. Kwa vyovyote vile, ndege mbili zilitua mapema siku ya Jumanne asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Machulishchy, karibu na Minsk. Ndege ambazo nambari zake za utambulisho zimeunganishwa na mkuu wa Wagner: moja kutoka Rostov-on-Don, nyingine kutoka Saint Petersburg.

Mapema Jumanne, rais wa Belarus alisema uasi huo ulitokana na usimamizi mbaya wa uhasama kati ya Wagner na jeshi la Urusi ambao uliendelea kukuwa kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni. "Hali ilitutoka, kisha tukadhani ilisuluhisha, lakini haikusuluhisha," Lukashenko amewaambia waandishi wa habari. "Hakuna mashujaa katika histori hii," ameongeza.

"Msimamo wangu (ni ufuatao): ikiwa Urusi itaanguka, tutabaki chini ya vifusi, sote tutakufa", amesema Bwana Lukashenko ili kuhalalisha misaada aliyotoa, kulingana na Moscow, kwa Kremlin, kutatua mgogoro huo, akiwa na Wagner. Rais wa Belarus pia amesema aliamuru jeshi lake kuwa "tayari" baada ya kuzuka kwa uasi wa kundi la wanamgambo Wagner nchini Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.