Washington: Wagner inasababisha 'maafa na uharibifu'
Uasi wa kikundi cha Wagner uliozinduliwa na kusitishwa nchini Urusi siku ya Jumamosi umeonyesha hatari inayosababishwa na kundi hili la mamluki katika nchi za Kiafrika ambazo zina ushirikiano nao, imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Imechapishwa:
"Ujumbe ambao tumepitisha kwa nchi hizi kwa umma na kibinafsi hapo zamani ni kwamba Wagner inapofika kundi la Wagner linapoingia katika nchi moja wapo, maafa na uharibifu vinashuhudiwa baadae," msemaji wa diplomasia ya Marekani Matthew Miller, almewaambia waandishi wa habari.
Urusi imeonyesha washirika wake wa Kiafrika kwamba Wagner inasababisha 'maafa na uharibifu'
.
Urusi: Putin atoa pendekezo kwa mamluki wa Wagner kujiunga na Jeshi au kwenda Belarus
Katika hotuba, Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa pendekezo kwa wapiganaji wa kundi la Wagner kujiunga na jeshi la Urusi au kumfuata kiongozi wao, Yevgeny Prigozhin, nchini Belarus.
Katika hotuba fupi ya televisheni, Vladimir Putin ameamua kuweka wazi msimamo wake kwa mamluki wa Wagner akiwaambia wachaguwe kwenda uhamishoni nchini Belarus wakiambatana na mkuu wao Yevgeny Prigozhin, huku akiwataka wajiunge na jeshi la Urusi.
Rais wa Urusi amesema Jumatatu kuwa amegiza "kuepusha damu" ni hali ambayo Ukraine na nchi za Magharibi walikuwa wakifurahia hali hiyo itokee wakati wa uasi wa kundi la Wagner. Amewashukuru Warusi kwa "uzalendo" wao na umoja wao. "Tangu kuanza kwa matukio, hatua zilichukuliwa kwa maagizo yangu ya moja kwa moja ili kuzuia damu kubwa zisimwagike," Valdimir Putin amesema.
Hakusema chochote juu ya hatima ya Yevgeny Prigozhin, wala waziri wake wa ulinzi, Sergei Choigou, au mkuu wa majeshi, Jenerali Valéry Guerassimov, ambao mkuu wa Wagner alikuwa akidai wauawe.