Pata taarifa kuu

Urusi: Wagner wataendelea na shughuli zao nchini Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kundi la Wagner liitaendelea kufanya kazi nchini Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati, mkuu wa diplomasia ya Urusi ametangaza siku ya Jumatatu Juni 26, 2023, ambaye pia amebainisha kwamba uasi wa kundi hili nchini Urusi hautaathiri uhusiano kati ya Moscow na marafiki zake. Washirika wa Wagner wanaofanya kazi nchini Mali na nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati "kama wakufunzi" wataendelea, "amesema Sergei Lavrov katika mahojiano na kituo cha RT.

Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, Aprili 20, 2023 huko Havana, Cuba.
Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, Aprili 20, 2023 huko Havana, Cuba. via REUTERS - RUSSIAN FOREIGN MINISTRY
Matangazo ya kibiashara

"Nimepokea simu kadhaa za mshikamano, ikiwa ni pamoja na simu kutoka kwa marafiki zangu wa Kiafrika. Juni 26, 2023, katika mahojiano na Kituo cha Urusi cha Today (RT), Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi alihojiwa juu ya wasiwasi unaowezekana katika baadhi ya za Afrika, baada ya uasi uliositishwa wa kundi la Wagner uliofanywa dhidi ya Kremlin Juni 23 na 24, 2023.

Sergei Lavrov ameelezea wasiwasi huu: "Sijaona hofu yoyote, sijaona mabadiliko yoyote katika mtazamo wa nchi za Kiafrika kwa Shirikisho la Urusi. "

Amekumbusha kuwa wanajeshi wa Wagner wanafanya kazi nchini Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati "kama wakufunzi". "Kazi hii bila shaka itaendelea," amesema kwenye kituo cha RT.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.