Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

CAR: Karibu waandamanaji 200 waounga mkono China na Urusi Bangui

Takriban watu 200 walmeshiriki katika maandamano ya kuunga mkono China na Urusi siku ya Jumatano huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, siku nne baada ya mauaji ya Wachina 9 katika eneo la uchimbaji madini katikati mwa nchi.

Waandamanaji walipeperusha bendera za Urusi na mabango yaliyoandikwa hasa "Tunaunga mkono China" au "Urusi ni Wagner, tunaipenda Urusi na tunawapenda Wagner", na kuweka shada la maua mbele ya Ubalozi wa China.
Waandamanaji walipeperusha bendera za Urusi na mabango yaliyoandikwa hasa "Tunaunga mkono China" au "Urusi ni Wagner, tunaipenda Urusi na tunawapenda Wagner", na kuweka shada la maua mbele ya Ubalozi wa China. © RFI/Carol Valade
Matangazo ya kibiashara

Mkusanyiko wa karibu watu 200 kwa wito wa Republican Front, chama chenye ushirikiano wa karibu na mamlaka, ulianza asubuhi na kumalizika saa sita mchana chini ya mnara wa ukumbusho kwa vikosi vya jeshi (FACA) na washirika wake kutoka Urusi.

Waandamanaji walipeperusha bendera za Urusi na mabango yaliyoandikwa hasa "Tunaunga mkono China" au "Urusi ni Wagner, tunaipenda Urusi na tunawapenda Wagner", na kuweka shada la maua mbele ya Ubalozi wa China.

Siku ya Jumapili, raia 9 wa China waliuawa katika shambulio kwenye eneo la uchimbaji madini katikati mwa nchi. Tume ya uchunguzi ilifunguliwa, huku Rais wa China Xi Jinping akitoa wito wa "adhabu kali" kwa wahalifu. "Tuko hapa kwa huzuni kufuatia mauaji ya wakazi wa China, ambao ni mshirika muhimu katika ujenzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati," Saint-Clair Banga-Bingui, naibu katibu wa chama cha Republican Front, ameliambia shirika la habari la AFP.

Bangui inashutumu Muungano wa Wazalendo wa Mabadiliko (CPC), muungano wa makundi ya waasi uliyoundwa mwezi Desemba 2020 kumpindua Rais Faustin Archange Touadéra, kwa kuhusika na shambulio hilo. Muungano wa waasi ulikanusha shutuma hizi, ukinyooshea kidole "mamluki wa Urusi wa Wagner" kwa ushirikiano wa serikali.

Mwishoni mwa maandamano, waandamanaji kadhaa walilipwa faranga za CFA 15,000 (sawa na euro 23) na chama cha Republican Front kwa ushiriki wao, amebainisha mwandishi wa habari wa AFP.

Jamhuri ya Afrika ya Kati, nchi ya pili kwa maendeleo duni duniani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, imekuwa uwanja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013, ambayo ni hatari sana katika miaka yake ya kwanza lakini ambayo imepungua kwa kasi tangu mwaka 2018. Mwishoni mwa 2020, makundi yenye nguvu zaidi kati ya makundi mengi yenye silaha ambayo wakati huo yaligawana theluthi mbili ya nchi hiyo yalianzisha mashambulizi kuelekea Bangui na Bw. Touadéra alitoa wito kwa Moscow kusaidia jeshi lake dhaifu.

Mamia ya wanamgambo wa Urusi walijiunga na mamia ya wenzao ambao wamekuwepo tangu mwaka nchini humo 2018, na kuifanya iwezekane kuzima mashambulizi ya waasi na kisha kuwarudisha nyuma kutoka sehemu kubwa ya maeneo na miji waliyodhibiti, lakini bila kuwa na uwezo wa kuweka uwepo na mamlaka ya taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati kila eneo walilodhibiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.