Pata taarifa kuu

CAR: Ufaransa yashtumiwa kwa jaribio la mauaji ya mmoja wa viongozi wa kundi la Wagner

Evgueni Prigojine, mwanzilishi wa kundi la Wagner, anaishutumu Ufaransa kwa jaribio la mauaji dhidi ya kiongozi wa wanamgambo wa Urusi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

Evguéni Prigojine anaishutumu Ufaransa kwa kuhusika na madai ya shambulio dhidi ya mwanamgambo wa kundi la wanamgambo la Wagner nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Evguéni Prigojine anaishutumu Ufaransa kwa kuhusika na madai ya shambulio dhidi ya mwanamgambo wa kundi la wanamgambo la Wagner nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Reuters/Reuters/Sergei Ilnitsky
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika rasmi la habari la TASS, Dmitri Siti alijeruhiwa vibaya siku ya Ijumaa Desemba 16 baada ya mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa katika kifurushi. Kifurushi ambacho alipokea katika kituo cha kitamaduni cha Urusi huko Bangui.

"Mkuu wa kituo cha kitamaduni cha Urusi alipokea kifurushi kisichojulikana. Alikifungua na mlipuko ukatokea,” shirika la habari la Urusi la TASS limeripoti. Dmitri Siti, mkuu wa kituo cha kitamaduni cha Urusi, kiongozi wa kampuni ya madini ya Lobaye Invest na mmoja wa viongozi wa kundi la Wagner katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, alilazwa hospitalini, taarifa ya vyombo vya habari inaendelea, na amepata 'majeraha mabaya'.

Kwenye ujumbe wa Telegraph, mwanzilishi wa kundi la wanamgambo wa Urusi, Evgueni Prigojine, alikuwa mwepesi kunyooshea Ufaransa kidole. Kulingana na kiongozi huyu, mshirika wa karibu wa Vladimir Putin, Dmitri Siti aliweza kusema kabla ya kupoteza fahamu kwamba aliona ujumbe ufuatao: "Hii ni zawadi yako kutoka kwa Wafaransa wote, Warusi wataondoka Afrika". Evgueni Prigojine amesema "aliiomba Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi kuzindua utaratibu wa kuitangaza Ufaransa kuwa taifa linalofadhili ugaidi, pamoja na uchunguzi wa kina kuhusu mbinu za kigaidi za Ufaransa na washirika wake wa Magharibi".

Mashambulizi yanalenga 'kuharibu' uhusiano kati ya Moscow na Bangui, Moscow imesema

Shambulio la bomu lililomjeruhi mwakilishi wa Urusi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati siku ya Ijumaa limelenga "kudhuru" maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, imeshutumu Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi.

"Tunalaani vikali kitendo hiki cha uhalifu ambacho kinalenga (...) kuharibu maendeleo ya uhusiano wa kirafiki kati ya nchi zetu mbili," imesema katika taarifa yake, bila hata hivyo kumtaja mtu anayeshukiwa kuwa mfadhili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.