Pata taarifa kuu
AFRIKA- UFARANSA- USALAMA

Wanajeshi wa Ufaransa wameondoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Wanajeshi wa mwisho wa Ufaransa, waliokuwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kulinda amani, wameondoka. 

Wanajeshi wa Ufaransa awali wakipiga doria jijini Bangui
Wanajeshi wa Ufaransa awali wakipiga doria jijini Bangui REUTERS/Emmanuel Braun
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja, baada ya Ufaransa hapo awali kutangaza kuwaondoa wanajeshi wake nchini humo, kufuatia hatua ya serikali ya Bangui kushirikiana na Urusi kwenye masuala ya usalama kwa kuruhusu kikosi cha mamluki wa Wagner. 

Ripoti zinasema wanajeshi hao wa mwisho wa Ufaransa, wapatao 47, waliokuwa wamesalia, wameondoka siku ya Alhamisi na walioneka wakiabiri ndege ya kijeshi jijini Bangui. 

Wanakuwa wanajeshi wa mwisho 130 waliokuwa wamesalia nchini humo, baada ya kumalizika kwa opersheni Sangaris iliyokamilika mwaka 2016 baada ya kutumwa kwa kikosi hicho mwaka 2013 kusaidia kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. 

Mwezi Oktoba, serikali ya rais Emmanuel Macron, ilitangaza kuondoa wanajeshi wake waliosalia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kufikia mwisho wa mwaka huu, baaada ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Paris na Bangui, kutetereka. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.