Pata taarifa kuu
URUSI-USHIRIKIANO

Lugha ya Kirusi kuanza kufundishwa katika vyuo vikuu Jamhuri ya Afrika ya Kati

Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Urusi umeimùarika katika nyanja mbalimbali: kiuchumi, kijeshi, lakini pia elimu ya juu na sasa mafundisho ya jumla ya lugha ya Kirusi yanatarajia kuanza katika vyuo vikuu vya nchi. Suala lililojadiliwa kati ya marais Vladimir Poutine na Faustin Ange Touadéra wakati wa mazungumzo ya simu.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Bangui.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Bangui. AFP - PACOME PABANDJI
Matangazo ya kibiashara

Hakuna Kihispania tena, karibu Kirusi! Mwanzoni mwa mwaka wa shule wa 2022, Lugha ya Kirusi itaanza kufundishwa katikavyuo vikuu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuanzia mwaka wa kwanza wa chuo kikuu.

Taarifa hii imegonga vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari nchini Urusi. Mipango inaendelezwa na walimu kutoka Moscow wanatarajiwa kuwasili katika mji mkuu waJamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui katika siku za usoni. Pengine suala hili litakuwa kwenye ajenda ya mkutano kati ya mawaziri wa elimu wa nchi hizo mbili. Mkutano ambao umepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Urusi, Moscow, mwezi Januari.

Jumatatu hii, Novemba 29, Kremlin pia iliifahamisha hilo. Vladimir Putin alizungumza kwa simu na Faustin Ange Touadéra, njia ya kuunga mkono ukaribu kati ya watu hao wawili, na kusisitiza kwamba rais wa Urusi alimpongeza mwenzake kwa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 63 ya uhutru wa  nchi hiyo (Desemba 1, 1958).

Kwa upande wake, rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alimshukuru mwenzake kwa "misaada mbalimbali" ambayo Urusi imetoa kwa nchi yake. Kremlin inataja elimu, biashara na mapambano dhidi ya Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.