Pata taarifa kuu
CAR

CAR: Makundi ya waasi kutengwa kwenye mazungumzo

Wadau mbalimbali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameshindwa kuafikiana kuhusu kushirikishwa kwa makundi ya waasi kwenye mazugumzo.

Kanisa la Sant'Egidio
Kanisa la Sant'Egidio CC wikimédia/LPLT
Matangazo ya kibiashara

Siku mbili za mazungumzo kati ya wawakilishi wa vyama vya siasa, mashirika ya kiraia na wawakilishi wa dini mbalimbali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yaliyoandaliwa na jumuiya ya Sant'Egidio, zilimalizika Jumatano wiki hii.

Mijadala hiyo ililenga kuandaliwa kwa mazungumzo yatakayojumuiya wadau mbalimbali nchini jamhuri yaliyoahidiwa, mazungumzo ambayo rais Faustin Archange Touadera aliahidi. Kwa ssa mazungumzo hayo yanaandaliwa, na zaidi ya yote kuhusu swala lenye utata mkubwa kuhusiana na kushiriki kwa makundi yenye silaha kwenye mazungumzo. Wadau mbalimbali wamegawanyika kuhusiana na kushirikishwa kwa makundi ya waasi kwenye mazungumzo.

Kulikuwa na mijadala mikali, mabishano makali - hadi jioni - hakuna makubaliano yaliyofikiwa na wadau walioshiriki mazungumzo hayo, lakini jumuiya ya Sant'Egidio kwa niaba ya washiriki ilitoa taarifa tu ya kawaida kuhusiana na mazungumzo "jumuishi" na "yasiyoingiliwa".

Licha ya idadi yao, wapinzani hawajaweza kubadilisha msimamo wa serikali ya Bangui ambayo haitaki makundi ya waasi kushirikishwa kwenye mazungumzo wakati hayajaweka silaha zao chini.

Makundi kadhaa ya waasi yameonyesha nia yao ya kushiriki katika mazungumzo hayo. "Labda yatafanyika ... kwa njia nyingine," mshiriki mmoja amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.