Pata taarifa kuu
CAR-HAKI

Kesi za kwanza za Mahakama Maalum ya Jinai kwa CAR kusikilizwa mwishoni mwa 2021

Kesi za kwanza za Mahakama Maalum ya Jinai kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati itafunguliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu, amesema, Alain Tolmo, afisa katika ofisi ya mwendesha mashitaka kwenye Mahakama Maalum ya Jinai kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CPS.

Rais Faustin Archangel Touadéra (katikati), wakati wa akizuru majengo ya CPS, ambayo yalizinduliwa rasmi Ijumaa, Novemba 13, 2020.
Rais Faustin Archangel Touadéra (katikati), wakati wa akizuru majengo ya CPS, ambayo yalizinduliwa rasmi Ijumaa, Novemba 13, 2020. Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mahakama hii ya pamoja, inayojumuisha majaji kutoka Jumuiya ya Afrika ya Kati na wa kimataifa, iliundwa mwaka 2015. Mahakama ya CPS inafuatilia uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari yaliyofanyika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwezi Januari 2003.

Mahakama hii maalum ya jinai ilianza shughuli yake tangu mwaka 2018. Lakini kwa sasa, iko tayari kushughulikia kesi hizo, kulingana na Alain Tolmo:

"Kuna faili kumi na mbili zilizo chini ya maagizo ya maandalizi, hivyo faili zilizo katika uchunguzi wa awali katika kiwango cha ngazi ya polisi kwa kutafuta ukweli. Kuna baadhi ya waranti zaidi ya ishirini zilizotolewa kwa kuwakamata wahusika, washiriki na wadhamini wa uhalifu dhidi ya binadamu. Ni ujumbe ambao tunatoa kwa wauaji na wafungwa wa baadaye ambao wanakabiliwa zaidi na adhabu na kukamatwa. Mahakama inafanya kazi. Siwezi kutoa majina yoyote hapa. Kuna ulinzi wa waathirika na mashahidi. "

Kwa mujibu wa afisa katika ofisi ya mwendesha mashitaka, kazi yao itawezesha Jamhuri ya Afrika ya Kati kuelekea Amani: "Hii ni kazi ya mahakama maalum ya jinai na inasaidia kuleta amani katika nchi hii ambayo inakabiliwa na mdororo wa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.