Pata taarifa kuu

Zaidi ya wakimbizi 15,000 kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati wakimbilia DRC

Zaidi ya raia 15,000 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliokimbia mapigano kati ya jeshi na waasi walivuka mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika muda wa siku 17, kulingana na ripoti iliyotolewa Alhamisi wikihii na afisa wa eneo hilo ambaye aliomba msaada kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada na mamlaka nchini DRC.

Kulingana na takwimu za shirika la moja wa Mataifa linalo hudumia wakimbizi, UNHCR, kwa jumla kuna wakimbizi 221,694 kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati nchini DRC. 114,008 wamepewa hifadhi huko Nord-Ubangi.
Kulingana na takwimu za shirika la moja wa Mataifa linalo hudumia wakimbizi, UNHCR, kwa jumla kuna wakimbizi 221,694 kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati nchini DRC. 114,008 wamepewa hifadhi huko Nord-Ubangi. Wikipedia/John Bompengo/MONUSCO
Matangazo ya kibiashara

"Kwa jumla, wakimbizi 15,059 kutoka Jaùhuri ya Afrika ya Kati, wanawake 1,637 na watoto 11,892, wamefika katika eneo la Bosobolo huko Ubangi Kaskazini, kulingana na takwimu zilizotolewa na Idara ya Uhamiaji ya DRC (DGM)", Mkuu wa eneo hilo Jeannot Haolo ameliambia shirika la habari la AFP.

"Watu hawa walianza kutoroka nchi yao kati ya Oktoba 10 na 27, yaani katika muda wa siku 17. Watu hawa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati wanakimbia mapigano kati ya vikosi tiifu, vinavyosonga mbele, na waasi wa makundi ya Seleka na Anti-Balaka. Mapigano ya hivi karibuni yalifanyika karibu na mji wa Kouango nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ", amebaini Bw. Haolo.

"Tunatoa wito kwa mamlaka na mashirika kutoa misaada kujitolea kwa ajili ya wakimbizi hawa," ameomba.

Eneo la Bosobolo liko katika jimbo la Nord-Ubangi kaskazini-magharibi mwa DRC, kwenye mpaka na CAR.

Kulingana na takwimu za shirika la moja wa Mataifa linalo hudumia wakimbizi, UNHCR, kwa jumla kuna wakimbizi 221,694 kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati nchini DRC. 114,008 wamepewa hifadhi huko Nord-Ubangi.

Mwezi Oktoba, wakimbizi 250 kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati walirejeshwa katika mji mkuuwa nciiyo, Bangui, ameliambia shirika la habari la AFP Michel Siazo, meya wa mji wa Zongo (Sud-Ubangi), jirani na Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.