Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

CAR: Touadéra aagiza "kusitishwa vita mara moja" dhidi ya waasi

Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, katika hotuba kwa taifa Ijumaa hii, Oktoba 15, ametangaza "kusitishwa vita mara moja" dhidi ya waasi na "kumalizika kwa operesheni za kijeshi na hatua zote za kijeshi katika maeneo yote nchini".

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, Septemba 17, 2021 huko Bangui.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, Septemba 17, 2021 huko Bangui. © Carol Valade / RFI
Matangazo ya kibiashara

Ahadi hii ilitolewa na serikali wakati wa kupitishwa kwa mpango wa kufuatwa wa Jumuiya ya Kanda ya Maziwa Makuu huko Luanda, ili "kutoa nafasi kwa amani", kulingana na rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

"Ninawatangazia leo jioni kumalizika kwa operesheni za kijeshi na hatua zote za kijeshi katika nchi nzima, kuanzia leo, Oktoba 15, 2021, saa sita usiku. Tangazo hilo limetolewa na rais wa Jamhuri kwenye redio ya taifa.

Hii ni ahadi iliyotolewa na serikali kwa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Kanda ya Maziwa Makuu (ICGLR), amesema Faustin-Archange Touadéra: "Ahadi ambayo inaonekana katika mpango wa serikali wa ajili ya amani, iliyotokana na mkutano wa mwisho wa jumuiy ahii ya kikanda. Viongozi wakuu wa muungano wa makundi ya waasi wa CPC, isipokuwa Nourredine Adam na Ali DARASSA, viongozi wa makundi ya FPRC na UPC, wamesaini mkataba wa kusitisha vitendo vyote vya kijeshi katika maeneo yote ya nchi. "

 "Nililazimika kutumia njia zote kuhakikisha usalama wa ria wa Jamhuri ya Afrika ya Kati" , alisema kwenye mahojiano na RFI leo asubuhi

"Sio uamuzi rahisi kuchukua," amekiri. Kukomesha mapigano kwa upande mmoja ni ujasiri, ikiwa ni lazima, ya nia yangu thabiti ya kupendelea njia ya mazungumzo na sio ya silaha, katika utatuzi wa mgogoro unaoikumba nchi yetu. "

Sababu za kibinadamu

Mkuu wa nchi anabainisha kuwa uamuzi wake hauzuii vikosi vya usalama vya ndani kudumisha utulivu, jeshi kujibu mashambulizi kwa kujihami, au Minusca kutekeleza majukumu yake.

Kusitishwa kwa mapigano pia ilmetokana na sababu za kibinadamu, amesema rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.