Pata taarifa kuu

Urusi itaendelea kufanya kazi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na au bila Wagner

Urusi itaendelea kufanya kazi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kundi la Wagner ambalo kwa sasa linasaidia Jeshi la nchi hiyo kupigana dhidi ya waasi, au kundi lingine, afisa mwandamizi wa katika ofisi ya rais katika nchi hii ya Afrika wa Kati ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu.

Kiongozi wa kundi la wanamgambo la Wagner Yevgeny Prigozhin.
Kiongozi wa kundi la wanamgambo la Wagner Yevgeny Prigozhin. AP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili linakuja muda mfupi baada ya mkuu wa diplomasia ya Urusi, Sergei Lavrov, kusema kwamba kundi hili la mamluki lililoanzisha uasi kwa muda mfupi siku ya Jumamosi dhidi ya Kremlin, "litaendelea" kufanya kazi nchini Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati, Moscow imekuwa ikidai kuwa ni "wakufunzi".

Jamhuri ya Afrika ya Kati imesaini (mnamo 2018) makubaliano ya ulinzi na Shirikisho la Urusi na sio Wagner, " amesema Fidèle Gouandjika, Waziri Mshauri wa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadéra, huku akiongeza: "Urusi ilifanyiana mikataba na kundi la Wagner, ikiwa Urusi haikubaliani tena na Wagner basi itatutuma kundi lingine. "

"Kesi kati ya Yevgeny Prigozhin (kiongozi wa Wagner) na (rais wa Urusi) Vladimir Putin haituhusu, ni mambo ya ndani nchini Urusi," amesema Bwana Gouandjika. Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kama "masuala mengine ya operesheni duniani", "wanaweza labda kubadilisha viongozi wa kundi hili lakini askari wa Wagner wataendelea kufanya kazi kwa niaba ya Shirikisho la Urusi", ameongeza.

Mamia ya mamluki wa Wagner waliwasili rasmi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mnamo 2018, kulingana na Moscow kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo, lakini hasa kwa sababu serikali ya Bw. Touadéra iliishtumu Ufaransa, kwa kuitena na kuunga mkono vikwazo vya silaha ambavyo vilizuia kuwapa silaha wanajeshi wake kutokomeza makundi mengi ya waasi yalio na theluthi mbili ya nchi hiyo tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya umwagaji damu mnamo 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.