Pata taarifa kuu

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Rais Touadéra atangaza kufanyika kwa kura ya maoni ya katiba

Faustin-Archange Touadéra ataitisha kura ya maoni ya katiba mnamo Julai 30. Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alitangaza hilo katika hotuba kwa taifa, iliyorushwa mtandaoni Jumanne hii alasiri, Mei 30. Mkuu wa Nchi anasema alishauriana na Spika wa Bunge la kitaifa na mkuu Mahakama ya Katiba.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, Septemba 17, 2021 mjini Bangui.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, Septemba 17, 2021 mjini Bangui. © Carol Valade / RFI
Matangazo ya kibiashara

Faustin-Archange Touadéra anadai "kuzingatia kwa uangalifu" sheria ya msingi ya 2016 ambayo alitumia kwa kuapa mara mbili. Hata hivyo, kulingana na rais huyo, Katiba ya sasa “inajumuisha vifungu vinavyoweza kuhatarisha maendeleo” ya nchi.

"Hii ndiyo sababu ya kutangazwa kwa Katiba hii, baadhi ya wanasiasa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na idadi kubwa ya raia wetu waliona haitoshi kwa sababu mbalimbali na tofauti, hasa kwa kuwa haipendekezi ufumbuzi unaofaa kwa sababu za migogoro ya kijeshi na kisiasa nchini. "

Katiba, kulingana na Faustin Archange Touadera, "haithibitishi kwa uwazi uhuru wa Serikali wala uhuru wa kitaifa, wala haki ya kujitawala ya watu," anaongeza, akisisitiza uhamasishaji wa kuunga mkono kura ya maoni ilioandaliwa katika miezi ya hivi karibuni na makundi yaliyo karibu na serikali. Hata hivyo maandamano mapya pia yalitangazwa kufanyika Jumatano, Mei 31.

Kulingana na yeye, kura hii ya maoni iko ndani ya mfumo wa "mageuzi ya kina ya nchi" ambayo alikuwa ameahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi wa urais wa 2020, na "itakuza maadili yetu, kuruhusu demokrasia yetu changa kuwa na nguvu zaidi" na "kuboresha utendaji kazi wa kawaida wa taasisi kwa msisitizo mkubwa katika uwazi na uwajibikaji”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.