Pata taarifa kuu

Faustin-Archange Touadéra: Shambulizi la Bossangoa ni la 'gaidi'

Katika mkesha wa kuadhimisha miaka 54 tangu kutangazwa kwa Jamhuri mwaka 1958, Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra alihutubia taifa siku ya Jumatano, Novemba 30 ambapo alizungumzia habari za kisiasa na usalama wa nchi hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, Septemba 17, 2021 mjini Bangui.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, Septemba 17, 2021 mjini Bangui. © Carol Valade / RFI
Matangazo ya kibiashara

Akiorodhesha matukio ya hivi majuzi ya usalama, Faustin-Archange Touadéra, hasa, alirejea kwenye mashambulizi ya mabomu katika kambi ya kijeshi ya Bossangoa usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu. Hakutoa maelezo zaidi, lakini aliita kitendo hicho cha "kigaidi". Rais Archange Touadéra alisema, mashambulio hayo yalilenga "maslahi ya kiuchumi", kiwanda cha mwisho cha kuchambua pamba nchini kiliathirika na mashambulizi haya.

Alikumbusha kuwa vyombo vya sheria vimefungua uchunguzi kubaini ndege hiyo iliyotekeleza mashambulizi hayo, asili yake na asili ya vilipuzi hivyo. Kulingana na vyanzo vya kidiplomasia, suala hili lilijadiliwa Jumanne huko Abuja kando ya mkutano wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Chad. Rais Touadéra aliomba ushirikiano wa Cameroon na hasa Chad, iliyonyooshewa kidole cha lawama na mashirika ya karibu na mamlaka ya Bangui. Inasemekana kwamba Ndjamena ilikubali kutoa ushirikiano wake.

Faustin-Archange Touadéra pia aliahidi katika hotuba yake "kudumisha uhusiano bora na [nchi] jirani kupitia sera ya ujirani mwema na kutoingilia kati masuala ya nchi yoyote". Wala hakusita kuwaongelea wapinzani wa mradi wowote wa marekebisho ya katiba. Vyama kadhaa pia vimekataa kushiriki katika sherehe rasmi ili kukemea hali ya usalama na kisiasa nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.