Pata taarifa kuu

Ndege kutoka nje ya nchi yashambulia kwa mabomu wanajeshi wa Afrika ya Kati

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati iimesema ndege iliyokuja na kwenda nchi jirani ilishambulia kwa mabomu kambi ya wanajeshi na washirika wao wa kijeshi kutoka Urusi jana Jumatatu, shambulio ambalo lilitokea kaskazini nchi, na kusababisha uharibifu pekee.

Mji wa Bossangao, kwenye ramani.
Mji wa Bossangao, kwenye ramani. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo "ilidondosha vilipuzi katika mji" wa Bossangoa "kuharibu kambi ya vikosi vyetu vya Ulinzi, kambi ya washirika wetu pamoja na kiwanda cha pamba", imeeleza taarifa ya serikali ambapo jeshi na mamia ya wapiganaji kutoka kundi la usalama la kibinafsi la Urusi Wagner linaendelea kupambana dhidi ya waasi. Bangui inawaita wanamgambo wa Kirusi kwa neno "Washirika".

Hii ni mara ya kwanza, angalau kutangazwa hadharani, kwamba shambulio hili linalodaiwa kufanywa na ndege hasimu limefanyika, angalau tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 2013.

"Vilipuzi hivi vilisababisha uharibifu mkubwa wa vifaa vya jeshi," taarifa hiyo imeongeza. "Ndege hii, baada ya kufanya uhalifu huu, ilichukua mwelekeo wa kaskazini kabla ya kuvuka mipaka yetu",  serikali imebainisha. Chad ndiyo ambayo iko kaskazini mwa Bossangoa, mji ambao si muda mrefu uliopita ulikuwa mikononi mwa waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.