Pata taarifa kuu

Mlinda amani wa Morocco auawa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Askari wa Umoja wa Mataifa kutoka Morocco aliuawa siku ya Alhamisi katika shambulio lililotokea kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, nchi iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 2013, umetangaza leo Ijumaa Umoja wa Mataifa, ambao haukuwatambua washambuliaji.

Mwanajeshi wa MINUSCA kutoka kikosi cha Morocco akipiga doria huko Bangassou, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Oktoba 10, 2021.
Mwanajeshi wa MINUSCA kutoka kikosi cha Morocco akipiga doria huko Bangassou, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Oktoba 10, 2021. © Carol Valade / RFI
Matangazo ya kibiashara

"Mlinda amani kutoka kikosi cha Morocco (...) aliuawa katika shambulio la Alhamisi asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Obo alipokuwa akilinda, na askari wengine wa kikosi chake, eneo la uwanja wa ndege", Umoja wa Mataifa umesema katika taarifa kwa vyombo vya habari. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), ambao umetuma kikosi cha kulinda amani tangu mwaka 2014, kikiwa na idadi ya zaidi ya wanajeshi 14,000 hivi leo.

MINUSCA inabainisha kuwa uchunguzi umefunguliwa ili kubaini "hali halisi" ya shambulio hili na kukumbusha kuwa "shambulio lolote dhidi ya maisha ya mlinda amani linaweza kuchukuliwa kuwa uhalifu wa kivita". Wanajeshi wa mwisho wa Umoja wa Mataifa waliouawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ni wanajeshi watatu wa Bangladesh waliouawa Oktoba 4 katika mlipuko wa bomu wakati gari lao lilipopita kaskazini magharibi mwa nchi.

Vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2013 wakati kundi la waasi ambao wengi wao walikuwa Waislamu, Séleka, lilipompindua rais François Bozizé, na kambi ya mkuu wa nchi aliyeondolewa madarakani ilianzisha vita kwa kulipiza kisasi wanamgambo walio wengi wanaojilinda, Wakristo na wenye imani kali, Anti-balaka. Umoja wa Mataifa ulituma wanajshi wake kuania mwaka 2014.

Mapigano kati ya makundi haya mawili, ambayo raia ndio waathiriwa wakuu, yalifikia kilele mnamo 2018 kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, hadi wakati huo mbaya sana, kupungua kwa kasi. Anti-balaka na Seleka wote wameshtakiwa na Umoja wa Mataifa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Mzozo huo umepungua kwa kiasi kikubwa tangu mwaka wa 2018, lakini makundi ya waasi kutoka Séleka na Anti-balaka kisha waligawana zaidi ya theluthi mbili ya nchi hadi mwanzoni mwa 2021. Tangu wakati huo, kwa wito wa Rais Faustin Archange Touadéra, Urusi ilituma mamia ya wanamgambo kutoka kundi la kibinafsi la usalama la Wagner ambao walisaidia kuyaondoa makundi yenye silaha kutoka katika maeneo mengi yaliyokuwa yakikalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.