Pata taarifa kuu

CAR: Wanamgambo 3 wa kundi la waasi la 3R wahukumiwa kwa 'uhalifu dhidi ya binadamu'

Watu watatu kutoka kundi la wanamgambo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wamehukumiwa siku ya Jumatatu kifungo cha kuanzia miaka 20 hadi maisha jela kwa "uhalifu dhidi ya binadamu" katika hukumu ya awali iliyotolewa na Mahakama Maalum ya Uhalifu (SCC), mahakama ya mseto ya mahakimu wa ndani na kimataifa.

Mahakama Maalum ya Jinai (CPS), katika ufunguzi wa kesi hiyo mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Aprili 19, 2022.
Mahakama Maalum ya Jinai (CPS), katika ufunguzi wa kesi hiyo mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Aprili 19, 2022. © RFI/Carol Valade
Matangazo ya kibiashara

Issa Sallet Adoum, Ousman Yaouba na Tahir Mahamat, kutoka kkundi la 3R walioshutumiwa kwa mauaji ya Mei 21, 2019, ya raia 46 katika vijiji vya kaskazini-magharibi, walipatikana na hatia ya " mauaji", "vitendo visivyo vya kibinadamu" na "vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji". Wa kwanza alihukumiwa kifungo cha maisha na mwingine kifungo cha miaka miwili hadi ishirini.

SCC, iliyoundwa mwaka 2015 na serikali chini ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa, ina jukumu la kushughulikia na kuhukumu uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa tangu 2003. Ilifungua kesi yake ya kwanza Aprili 25, ambayo iliahirisha kusikilizwa kwa mara ya kwanza, bila washtakiwa kusikilizwa, kutokana na kutokuwepo kwa mawakili wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.