Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Wachina tisa wauawa katika shambulizi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Wachina tisa wameuawa katika eneo la uchimbaji madini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, shambulio lililolaaniwa na Rais wa China Xi Jinping ambaye ametoa wito Jumatatu 'kuwaadhibu vikali' wahalifu.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadera.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadera. AFP PHOTO/ SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea Jumapili mwendo wa saa kumi na moja alfajiri kwa saa za  Afrika ya Kati katika eneo la Bambari, katikati mwa nchi hiyo ya Kiafrika, meya wa wilaya hiyo, Abel Matchipata, ameliambia shirika la habari laAFP. "Tumehesabu miili tisa na majeruhi wawili," amesema.

Kulingana na Abel Matchipata, wahanga ni raia wa China wanaofanya kazi kwenye eneo la uchimbaji madini la "Gold Coast Group", lililoko kilomita 25 kutoka eneo hilo na ambalo lilishambuliwa na "watu wenye silaha".

China imethibitisha idadi hiyo Jumatatu, ikibainisha "wawili waliojeruhiwa vibaya", lakini bila kutoa maelezo zaidi juu ya mazingira ya shambulio hili, ambalo halijadaiwa hadi sasa. Xi Jinping "ametoa wito wa kufanya kila juhudi kuwatibu waliojeruhiwa" pamoja na "kuwaadhibu vikali wauaji kwa mujibu wa sheria," Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema katika taarifa.

"Mbali na mji mkuu Bangui, kiwango cha hatari ya usalama katika maeneo mengine ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ni nyekundu, ambayo ni kusema kiko juu sana", imesisitiza wizara hiyo, ikitoa wito kwa raia wa China "kuhama haraka iwezekanavyo" maeneo hatari.

'Shambulio la kijinga na la kishenzi"

Miili ya wahanga wa shambulio hilo ilihamishiwa katika Hospitali ya Urafiki mjini Bangui, ambako balozi wa China, Li Qinfeng, amezuru na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sylvie Baipo Temon, amebainisha mwandishi wa habari wa AFP.

Muungano wa Wazalendo wa Mabadiliko (CPC), muungano wa makundi ya waasi ulioundwa mwezi Desemba 2020 kumpindua Rais Faustin Archange Touadéra, umekanusha kuhusika kwa vyovyote katika shambulio hilo la Jumapili. Ulilaani  kitendo cha "kijinga na cha kinyama", hata hivyo muungano huo umewashutumu "mamluki wa Urusi (wa shirika la kijeshi) Wagner" kwa kuhusika na shambulio hilo.

Jamhuri ya Afrika ya Kati, nchi ya pili kwa maendeleo duni duniani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, imekuwa uwanja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013, ambayo ni hatari sana katika miaka yake ya kwanza lakini ambayo imepungua kwa kasi tangu mwaka 2018. Mwishoni mwa mwaka 2020, makundi yenye nguvu zaidi kati ya makundi mengi yenye silaha ambayo yaligawana theluthi mbili ya eneo hilo yalianzisha mashambulizi mjini Bangui muda mfupi kabla ya uchaguzi na Bw. Touadéra alitoa wito kwa Moscow kulisaidia jeshi lake lililodhoofika.

Mamia ya wanamgambo wa Urusi walijiunga na mamia machache ambayo tayari yamekuwepo tangu 2018, na hivyo kuwezesha, katika miezi michache, kuzima mashambulizi ya waasi, kisha kuwafukuza kutoka sehemu kubwa ya maeneo na miji waliyodhibiti, lakini bila ya kuweza kuweka upya kila mahali mamlaka ya Taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.