Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron azuru Mongolia, kwa mara ya kwanza kwa rais wa Ufaransa

Baada ya mkutano wa kilele wa G7 huko Hiroshima, nchini Japan, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anazuru Mongolia kwa ziara fupiya kiserikali Jumapili Mei 21. Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Ufaransa aliye madarakani kuzuru Mongolia, nchi isiyo na bandari kati ya China na Urusi.

Mongolia inajaribu kujikomboa kutoka kwa utegemezi wa majirani zake, China na Urusi. Hapa, mlinzi wa mpaka anakagua magari yanayowasili kutoka Urusi kwenye mpaka na nchi huko Altanbulag mnamo Septemba 25, 2022.
Mongolia inajaribu kujikomboa kutoka kwa utegemezi wa majirani zake, China na Urusi. Hapa, mlinzi wa mpaka anakagua magari yanayowasili kutoka Urusi kwenye mpaka na nchi huko Altanbulag mnamo Septemba 25, 2022. © Byambasuren Byamba-ochir, via AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Hiroshima, Vincent Souriau

Ikulu ya Élysée inachukulia Mongolia kama kielelezo cha serikali ya kiliberali, nchi yenye uzoefu katika siasa kwa viongozi kupishana na kukabidhiana madaraka kwa amani, hali ambayo hufanya uchaguzi kufanyika kwa uwazi. Lakini pia ni nchi isiyo na bahari kati ya nchi mbili zenye zenye nguvu katika ukanda huo : Urusi na China.

Hata hivyo, nchi hii inataka inatazamia kuelekea katika mfumo wingine: kubadilisha ushirikiano wake ili kupunguza utegemezi wake kwa majirani zake.

Mamlaka ya Ufaransa inakaribish ahali hiyo na inatarajia kujikita katika masuala mbalimbali hasa juu ya nishati. Kwa upande mmoja, kuna migodi ya uranium ya Kimongolia na kwa upande mwingine, ujuzi wa Ufaransa katika suala la nishati mbadala. Kwa sababu Mongolia inahitaji kupunguza kaboni, inategemea 90% ya makaa ya mawe ili kuzalisha umeme wake. Ufaransa inaona katika fursa hii umuhimu wa ushirikiano katika sekta ya mazingira.

Katika ngazi ya kimkakati, Paris inazingatia kwamba Wamongolia, kama majirani wote wa Urusi, lazima wapewe kitu muhimu ili kulegeza kikwazo kilichowekwa na Moscow.

Kwa sehemu moja ni aina ya utambuzi wa tabia ya Mongolia katika ukanda huo. Ni nchi ambayo inatofautishwa na kielelezo ambacho ni cha kidemokrasia na kiliberali na ambacho kinatofautiana na nchi nyingine za ukanda huo na ambayo pia inakuza sera ya kigeni ambayo inalenga kupata nafasi ya kufanya kazi katika mazingira ya kikanda ambayo yana vikwazo vingi. hasa kwa sababu ya kutengwa kwake kati ya China na Urusi, kwa nia ya mamlaka ya Mongolia kugawanya uhusiano ambao wanaweza kuwa nao na majirani zao, kwa mfano makampuni ya China yanahusika katika maendeleo ya baadhi ya mali ya madini nchini Mongolia; na kwamba wadau kutoka Ufaransa ambao pia wanakuja kunyonya rasilimali katika ardhi ya Mongolia, hiyo inafanya uwezekano wa kusawazisha uhusiano kidogo na kuruhusu mamlaka ya Kimongolia kuwa na uhuru zaidi na kutokuwa tegemezi kwa majirani zake pekee. Kuna uhusiano mwingi na Japan, na Korea Kusini, India, na Ufaransa, mamlaka ya Kimongolia pia inatumai maendeleo ya ushirikiano, iwe katika sekta ya madini, katika sekta ya nishati au hata katika sekta ya kilimo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.