Pata taarifa kuu

Miungano ya wafanyakazi nchini Ufaransa kufanya maandamano mengine Juni 6

NAIROBI – Miungano ya wafanyakazi nchini Ufaransa, imesema itaitisha maandamano mengine ya umma mwezi ujao, kupinga sheria ya mageuzi ya pensheni iliyoidhinishwa na rais Emmanuel Macron.

Wanafunzi wakiimba wakati wa maandamano huko Paris
Wanafunzi wakiimba wakati wa maandamano huko Paris AP - Thibault Camus
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri siku moja tu baada ya mamia kwa maelfu kujitokeza na kuandamana kupinga sheria hiyo.

Miungano hiyo imesema maandamano hayo yatafanyika Juni 6, siku kadhaa kabla ya wabunge kujadili mswada ambao utafutilia mbali mapendekezo ya kuongeza umri wa kustaafu, ambayo yalipitishwa bila mawaziri wa Macron kupiga kura.

Kwa mujibu wa miungano hiyo, licha ya kwamba watahudhuria majadiliano mapya na baraza la mawaziri kuhusu maswala mbalimbali, watasisitiza nia yao ya kupinga mageuzi ya pensheni.

Kuna ukaidi mkubwa na mazungumzo yanaweza tu kuanza tena ikiwa serikali itaonyesha kwamba hatimaye iko tayari kuzingatia misimamo ya vyama vya wafanyakazi, miuangano hiyo imeongeza.

Waziri wa usalama wa kitaifa wa Ufaransa, Gerald Darmanin, amesema katika maandamano ya Jumatatu, Mei 1, watu 540 walikamatwa nchini ikiwa ni pamoja na 305 huko Paris.

Darmanin amesema maafisa watatu wa polisi walijeruhiwa katika ghasia za hapo jana, na kwa sasa mmoja yuko hospitalini akiuguza majeraha, baada ya kugongwa usoni na kimiminika cha Molotov cocktail, kinachoweza kushika moto.

Katika maandamano hayo, waandishi wawili wa habari pia walijeruhiwa akiwemo mpiga picha wa AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.