Pata taarifa kuu

Maelfu ya raia wameandamana nchini Ufaransa kupinga sheria mpya ya pensheni

NAIROBI – Nchini Ufaransa, maelfu ya waandamanaji wenye hasira, wameandamana katika miji mbalibali nchini humo, kuendelea kupinga sheria mapya ya pensheni iliyotiwa saini mwezi uliopita na rais Emmanuel Macron.

Wafanyakazi wa umma nchini Ufaransa wanaendelea kupinga sheria mpya kuhusu pensheni
Wafanyakazi wa umma nchini Ufaransa wanaendelea kupinga sheria mpya kuhusu pensheni AP - Aurelien Morissard
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi wakiongozwa na viongozi wa vyama vinavyotetea maslahi yao, wametumia sikukuu ya wafanyakazi ya Mei Mosi, kuendeleza kushinikiza na kuonesha upinzani wao dhidi ya sheria hiyo, huku wakiapa kuendelea kupinga mageuzi hayo.

Miongoni mwa mabadiliko yanayopingwa na wafanyakazi katika nchi hiyo ni pamoja na kuongeza umri wa watu kuusatafu kutoka miaka 62 hadi 64.

Maafisa wa polisi jijini Paris, walitumia ndege zisizokuwa na rubani, kuhakikisha kuwa waandamanaji hawazui fujo na uaharibifu wa mali, kama ilivyoshuhudiwa wakati wa maandamano yaliyopita.

Hata hivyo, katika mji wa Toulouse, Kusini mwa Ufaransa, polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji, huku wakiteketeza moto gari katika mji wa Lyon.

Hata kabla ya kufanyika kwa maandamano haya, raus Macron aliapa kuwa hatabadilisha sheria hiyo, ambayo imemfanya kupoteza umaarufu wa kisiasa katika kipindi cha pili cha uongozi wake, huku akiahidi maslahi bora kwa wafanyakazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.