Pata taarifa kuu

Rais Macron ametia saini mswada unaopendekeza mageuzi ya pensheni kuwa sheria

NAIROBI – Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametia saini mswada unaopendekeza mageuzi kuhusu pensheni kuwa sheria, licha ya upinzani mkali kutoka kwa wafanyakazi wa umma, ambao kwa miezi mitatu wamekuwa wakiandamana na kugoma.

 Emmanuel Macron rais wa Ufaransa
Emmanuel Macron rais wa Ufaransa AP - Lewis Joly
Matangazo ya kibiashara

Baada ya hatua hiyo, sheria hiyo mpya, imechapishwa kwenye gazeti la serikali.

Wapinzani wake, wamemshtumu kwa kutia saini, mswada huo kuwa sheria usiku wa manane, hatua iliyokuja baada ya Mahakama ya Katiba kuidhinisha mswada huo.

Mwanasiasa kutoka chama cha Kisosholisti Olivier Faure, amesema Macron kwa kutia saini mswada huo, ni kudharau sauti na maoni ya waandamanaji.

Miongoni mwa kipengele tata kwenye sheria hii tata, ni kuongeza muda wa wafanyakazi wa umma kustaafu kutoka umri wa miaka 62 hadi 64.

Rais Macron amekuwa akitetea mabadiliko hayo akisema ni muhimu ili kuepusha serikali kushindwa kukusanya fedha za kuwalipa waastafu inayokaridiwa kuwa Euro Bilioni 13.5 ifikapo mwaka 2030.

Vyama vya wafanyakazi vimelaani uamuzi huo wa rais Macron na kusema kuwa suala hilo halijaisha na kutangaza maandamano na mgomo wa nchi nzima, tarehe 1 Mwezi wa tano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.