Pata taarifa kuu

Burma: Utawala wa kijeshi watangaza kuwasamehe zaidi ya wafungwa 3,000 kwa ajili ya Mwaka Mpya

Serikali ya Burma imetangaza Jumatatu kuachiliwa kwa wafungwa zaidi ya 3,000 kwa ajili ya hafla ya Mwaka Mpya wa Kibudha, bila kutaja kama msamaha huu unatumika kwa wale waliokamatwa kama sehemu ya ukandamizaji wake dhidi ya upinzani.

Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa serikali ya kijeshi nchini Burma, wakati wa mkutano wa Baraza la Ulinzi na Usalama la Kitaifa mnamo Jumanne, Januari 31, 2023 huko Naypyidaw.
Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa serikali ya kijeshi nchini Burma, wakati wa mkutano wa Baraza la Ulinzi na Usalama la Kitaifa mnamo Jumanne, Januari 31, 2023 huko Naypyidaw. AP
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi mkuu wa utawala wa kisheji Min Aung Hlaing "amewasamehe wafungwa 3,015 kwa ajili ya kusherehekea Mwaka Mpya nchini Burma, kwa amani ya raia, na kwa misingi ya kibinadamu", huduma ya mawasiliano ya jeshi lililo madarakani imesema. 

Katika tukio la ukiukwaji mpya wa sheria, wale walioachiliwa watalazimika kutumikia kifungo kilichobaki na kuongezewa adhabu, imeongeza. 

Taarifa hiyo haikubainisha ikiwa wapinzani wa serikali ya kijeshi, au waandishi wa habari waliofungwa kwa kuandika habari kuhusu mapinduzi, wanahusika na msamaha huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.