Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa: Utawala wa kijeshi wa Burma 'unafanya vita dhidi ya raia wake'

Katika ripoti iliyochapishwa Ijumaa hii, Machi 3, Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa inashutumu wanajeshi madarakani huko Burma kwa "kusababisha mgogoro" kwa chanzo cha janga la kibinadamu.

Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Burma, katika mkutano wa Baraza la Ulinzi na Usalama la Kitaifa Jumanne Januari 31, 2023 huko Naypyidaw.
Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Burma, katika mkutano wa Baraza la Ulinzi na Usalama la Kitaifa Jumanne Januari 31, 2023 huko Naypyidaw. AP
Matangazo ya kibiashara

Miaka miwili baada ya mapinduzi ya Februari 1, 2021 ambayo yaliipindua serikali ya raia ya Aung San Suu Kyi, hali 'inazidi kuwa mbaya,' Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba jeshi linafanya kazi katika "kutokujali kabisa na bila kuadhibiwa".

Katika ripoti iliyochunguza miaka miwili ya kwanza tangu mapinduzi ya kijeshi, Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kwamba watu wasiopungua 2,940 waliuawa, karibu 30% walikutwa wamefariki wakiwa kizuizini.

WHata hivyo, idadi halisi ya vifo labda ni kubwa zaidi, amebaini James Rodehaver, mkuu wa Ofisi ya Kamishna Mkuu nchini Burma. "Wanachofanya sasa ni kwamba wanawachukulia raia wa Burma kama wapinzani wao na maadui zao," amesema. Muna jeshi ambalo hufanya vita dhidi ya raia wake. "

Ameongeza kuwa, vikosi vya jeshi sasa vinapigana kikamilifu zaidi katika pande kumi na tatu tofauti. "Jeshi linazidi kunyooshewa kidole kwa uhalifu huo," amesema wakati wa mkutano wa waandishi wa habari huko Geneva. 

Ripoti za Umoja w Mataifa zinaonyesha kuwa karibu nyumba 39,000 kote nchini zimechomwa moto au kuharibiwa wakati wa operesheni za kijeshi tangu mwezi Februari 2022, "hali ambayo ni zaidi ya 1,000" ikilinganishwa na mwaka 2021. Jeshi na polisi wamewakamata watu 17,572 tangu mapinduzi, kulingana na ripoti hiyo.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.