Pata taarifa kuu

Takriban watu 50 wauawa katika shambulio la Jeshi la Anga la Myanmar dhidi ya waasi

Takriban watu 50 wameuawa na wengine 70 kujeruhiwa katika shambulio la Jeshi la Wanahewa la Myanmar dhidi ya kundi la waasi, msemaji wa kundi hilo amesema Jumatatu.

Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa utawala wa kijeshi ambao umechukua mamlaka nchini Myanmar tangu Februari 2021, hapa ilikuwa mwezi Machi 2021.
Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa utawala wa kijeshi ambao umechukua mamlaka nchini Myanmar tangu Februari 2021, hapa ilikuwa mwezi Machi 2021. REUTERS - Stringer .
Matangazo ya kibiashara

"Jumapili mwendo wa saa mbili na dakika arobaini usiku, ndege mbili za kijeshi za Myanmar zilishambulia" hafla iliyoandaliwa na Jeshi linalotetea uhuru wa Kachin (KIA), Kanali Naw Bu ameliambia shirika la habari la AFP. "Takriban watu 50 wameuawa, wakiwemo maafisa wa KIA na raia," amesema na kuongeza kuwa takriban watu 70 wamejeruhiwa.

Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kuwa hadi wanajeshi na raia 60 wa KIA wamepoteza maisha. Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Myanmar imesema "imesikitishwa na kuhuzunishwa na ripoti za mashambulizi ya anga yaliyotokea Hpakant, Jimbo la Kachin".

"Ripoti za awali zinaonyesha kuwa zaidi ya raia 100 wanaweza kuwa wameathiriwa na mashambulizi hayo," Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Myanmar imebaini katika taarifa yake. "Pia kumeripotiwa vifo vingi," imeongza. Kwa upande wake, msemaji wa serikali ya Myanmar alikataa kutoa maoni kuhusu habari hii. Kumekuwa na mapigano ya mara kwa mara kati ya KIA na jeshi kwa miongo kadhaa na mapigano makali yalizuka kufuatia mapinduzi ya mwaka jana nchini Myanmar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.