Pata taarifa kuu

Wakimbizi wa Rohingya waadhimisha "mauaji ya kimbari" ya watu wao yaliyofanywa na Burma

Miaka mitano iliyopita, takriban Warohingya 750,000, Waislamu wachache wasio na utaifa na wanaoteswa nchini Burma, walitorokea nchini Bangladesh, wakimbia dhuluma za jeshi la Burmadhidi yao. Maelfu kadhaa kati yao wameandamana Alhamisi hii, Agosti 25 kuadhimisha miaka mitano ya ukandamizaji.

Warohingya waandamana kwenye kambi ya wakimbizi karibu na Cox's Bazar mnamo Novemba 15, 2018.
Warohingya waandamana kwenye kambi ya wakimbizi karibu na Cox's Bazar mnamo Novemba 15, 2018. AP - Dar Yasin
Matangazo ya kibiashara

Maelfu kadhaa ya Warohingya, wakimbizi katika kambi za muda kusini-mashariki mwa Bangladesh, wameandamana Alhamisi hii, Agosti 25 kuadhimisha mwaka wa tano wa mauaji ya watu wao nchini Burma, ambayo wanayaelezea kama "mauaji ya halaiki".

Pamoja na mabango na kauli mbiu, jamii hii yenye Waislamu wengi imekusanyika katika eneo la Cox's Bazar, kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani.

Wengi walichukua fursa hiyo kutaka kufutwa kwa sheria ya Burma ya mwaka 1982 iliyowanyima uraia katika nchi yao ya asili, yenye watu wengi kutoka jamii ya Wabudha. Maelfu haya ya Warohingya, wengi wao wakiwa wamevalia longyi  (sarong) na shati ya kitamaduni ya Kiburma, walijipanga kwa amani kwa ajili ya "Siku hii ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari".

Wakimbizi milioni moja

Miaka mitano baada ya ukandamizaji huo kutokea nchini Burma, karibu wakimbizi milioni moja wa Rohingya bado wanaishi wakiwa wamejazana kwenye kambi hizi chafu, huko Cox's Bazar na katika kisiwa cha Bahsan Char. Mafuriko, ukosefu wa usalama, uwepo wa magenge, hali ya maisha ni ya kusikitisha, wakati kurejea kwa Warohingya huko Arakan nchini Burma kumeathiriwa zaidi, hasa tangu mapinduzi ya kijeshi ya serikali ya Burma ambayo yaliiingiza nchi hii katika machafuko.

"Watu katika kambi ni marufuku kufanya kazi. Wako chini ya vikwazo muhimu sana vya uhuru. Ni muhimu kwamba mashirika ya kimataifa yanaweza kujali hatma ya watu hawa katika kambi za wakimbizi, " Alexandra de Mersan, mwanaanthropolojia, mtafiti na mwalimu katika taasisi ya INALCO amebaini akihojiwa na mwandishi wa RFI Jelena Tomic.

Warohingya wengi wanaendelea kukimbilia Malaysia hasa, moja ya nchi jirani. "Warohingya waliokuwa Arakan pia walipata aina ya kifungo, lakini ni kifungo katika ngazi ya eneo lao, ambapo huko wanaishi katika mazingira ya uasherati, hatari na vurugu za kisaikolojia, na muda mfupi wa vurugu. Ni maisha magumu sana ya kila siku, "ameongeza Alexandra de Mersan.

Kuzorota kwa hali ya maisha nchini Burma

Takriban Warohingya 600,000 ambao wamesalia nchini Burma wanaishi, kwa upande wao, katika hali ngumu sawa. Wamewekwa katika kambi baada ya kuhamishwa katika mawimbi ya ghasia za hapo awali au kuishi maisha ya hatari kwa huruma ya wanajeshi na walinzi wa mpaka.

Wengi wao wananyimwa uraia na wanawekewa vikwazo vya kutembea, kupata huduma za afya na elimu, matibabu ambayo, kulingana na shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, ni sawa na "ubaguzi wa rangi".

Kurejea kwa wanajeshi madarakani mwaka jana kumedidimiza zaidi matumaini ya njia ya kuelekea uraia au hata kulegeza masharti ya sasa.

Ukandamizaji wa serikali dhidi ya upinzani "umezidisha kuzorota kwa hali ya kibinadamu, hasa kwa jamii za makabila madogo na ya kidini, pamoja na Rohingya", Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Jumatano. Kundi hili "limesalia miongoni mwa watu walio hatarini zaidi na waliotengwa nchini", aliongeza.

Kiongozi wa utawala wa kijeshi Min Aung Hlaing, ambaye aliongoza vikosi vya jeshi wakati wa ukandamizaji wa 2017, aliita utambulisho wa Rohingya "wa kufikirika". Kwa wale walio katika kambi, hata kurudi nyumbani ni jambo lisilowezekana, amesema Marjan Besuijen kutokasirika lisilo la kiserikali la Madaktari wasi na Mpiaka, MSF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.