Pata taarifa kuu

UN: Bado kuna ushahidi wa uhalifu dhidi ya binadamu Burma

Kuna ushahidi tosha kwamba uhalifu dhidi ya binadamu umefanywa nchini Burma tangu mapinduzi ya mwaka jana, wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema Jumanne.

Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa utawala wa kijeshi ambao umechukua mamlaka nchini Burma tangu Februari 2021, hapa ilikuwa mwezi Machi 2021.
Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa utawala wa kijeshi ambao umechukua mamlaka nchini Burma tangu Februari 2021, hapa ilikuwa mwezi Machi 2021. REUTERS - Stringer .
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake ya kila mwaka, Mfumo Huru wa Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kwa Burma unabaini kuwa wanawake na watoto ndio hasa walengwa.

"Kuna ushahidi mkubwa kwamba tangu jeshi lichukue mamlaka mnamo mwez iwa Februari 2021, uhalifu umetendwa nchini Burma kwa kiwango kikubwa na kwa njia ambayo inajumuisha shambulio la jumla na la kawaida dhidi ya raia," shirika hilo limesema katika taarifa. .

Taasisi hii Iliyoundwa na Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mnamo mwezi wa Septemba 2018, inalenga kukusanya ushahidi juu ya uhalifu mbaya zaidi kwa kuzingatia uwezekano wa kesi za jinai.

Ubakaji na uhalifu dhidi ya watoto

"Uhalifu dhidi ya wanawake na watoto ni miongoni mwa uhalifu mbaya zaidi wa kimataifa, lakini pia kihistoria hauripotiwi na haujachunguzwa," Nicholas Koumjian, Mkuu wa Mfumo Huru wa Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa, amesema katika taarifa.

"Wahusika wa uhalifu huu lazima wajue kwamba hawawezi kuendelea kutenda bila kuadhibiwa, tunakusanya na kuhifadhi ushahidi ili siku moja wawajibishwe," ameongeza.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo kwa wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, "uhalifu wa kijinsia na ule unaohusiana na kijinsia, ikiwa ni pamoja na ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia, pamoja na uhalifu dhidi ya watoto umekuwa ukifanywa na maafisa wa vikosi vya usalama na makundi yenye silaha".

Kulingana na ripoti hiyo, watoto waliteswa, waliajiriwa kwa nguvu na kuzuiliwa kiholela.

Tangu mapinduzi ya Februari 1, 2021 yaliyompindua kiongozi wa zamani wa kiraia Aung San Suu Kyi, utawala wa kijeshi umekuwa ukifanya msako mkali dhidi ya wapinzani wake, huku zaidi ya raia 2,100 wakiuawa na karibu 15,000 kukamatwa, kulingana na shirika moja lisilo la kiserikali katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.